Vita Ethiopia

Umoja wa mataifa waonya kuhusu Mzozo wa kibinadamu nchini Ethiopia

Kenya na Uganda zimetoa wito wa majadiliano ya amani kusuluhisha mzozo huo

Muhtasari

 

  • Mapigano yalitokea baada ya serikali ya Ethiopia kushutumu chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) , Kinachodhibiti Tigray, kuwa wahaini.
  • Serikali ya Ethiopia haijaonesha mpango wa kufanya mazungumzo na TPLF ambayo inaiona kama "kundi" ambalo njama yake ni kuvuruga katiba ya nchi hiyo.

 

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

 

Mzozo wa wiki mbili katika jimbo la Tigray lililo Kaskazini mwa Ethiopia sasa umekuwa "mzozo wa kibinadamu", Umoja wa Mataifa umesema.

Karibu watu 27,000 wamekimbilia nchi jirani ya Sudan, na UN inasema wafanyakazi wake wamezidiwa.

Mapigano yalitokea baada ya serikali ya Ethiopia kushutumu chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) , Kinachodhibiti Tigray, kuwa wahaini.

TPLF kinaona kama serikali ya Ethiopia ni batili.

Mzozo umegharimu maisha ya mamia ya watu, lakini kupata taarifa kutoka Tigray imekuwa vigumu, kwa kuwa hakuna mawasiliano eneo hilo.

Kenya na Uganda zimetoa wito wa majadiliano ya amani kusuluhisha mzozo huo.

Serikali ya Ethiopia haijaonesha mpango wa kufanya mazungumzo na TPLF ambayo inaiona kama "kundi" ambalo njama yake ni kuvuruga katiba ya nchi hiyo.

Siku ya Jumanne Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisema oparesheni ya kijeshi katika jimbo la Tigray inaingia "awamu ya mwisho", akiongeza kuwa muda wa makataa ya siku tatu uliyopewa makundi yaliyojihami katika eneo la Tigray umeisha.

Umoja wa Mataifa umewema nini?

 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia wakimbizi UNHCR, limesema kuwa "mzozo mkubwa wakibinadamu unaendelea kushuhudiwa" huku maelfu ya watu wakitoroka mapigano yanayoendelea katika eneo la Tigray.

Shirika hilo liko tayari "kutoa msaada katika eneo la Tigray likipata nafsi kufika huka hali ya usalama ikiruhusu" Msemaji Babar Baloch aliwaambia wanahabari mjini Geneva.

"Huenda kukawa watu wengi waliofurushwa makwap ndani ya Tigray na hiyo ni hali tutakayopatia kipaumbele na tunajiandaa vilivyo kuwasaidia," Jens Laerke, msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshirikisha masuala ya kibinadamu (OCHA), aliwaambia wanahabari.

Katika ujumbe wa Facebook aliwashukuru wapiganaji wa TPLF ambao walitumia muda wa siku tatu ya makataa kujiunga na upande wa serikali lakini hakusema ni wangapi waliofanya hivyo.

Amesema serikali yake "iko tayari kuwapokea na kuwaunganisha katika jamii Waethiopia wanzao waliokimbilia nchi jirani".

Bwana Abiy pia aliwaongoza Waethiopia katika hatua ya kuwashukuru wanajeshi wa Ethiopia kwa kushiriki katika oparesheni ya Tigray.

TPLF ilitawala jeshi la Ethiopia na maisha ya kisiasa kwa miongo kadhaa kabla ya Bw Abiy kuingia mamlakani mwaka 2018 na kupitisha mageuzi mkubwa.

Mwaka jana Bw Abiy alivunja muungano tawala , unaojumuisha vyama vilivyoundwa kwa misingi ya kikabila , na kuviunganisha katika chama kimoja, national party, the Prosperity Party, ambacho TPLF walikataa kujiunga.

Utawala wa Tigray unayaona mageuzi ya Bw Abiy kama jaribio la kujenga mfumo serikali moja na kuharibu mfumo uliopo sasa wa shirikisho.

Pia hukasirishwa na kile inachokiita urafiki wa waziri mkuu na rais wa Eritrea Isaias Afwerki "usiokuwa na kanuni "

Bw Abiy alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2019 kwa juhudi zake za kuleta amani kwa kumaliza mzozo wa muda mrefu wa nchi yake na Eritrea.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu anaamini kuwa maafisa wa TPLF wanadharau mamlaka yake.

Bw Abiy alimuru mashambulio ya kijeshi dhidi ya TPLF baada ya kusema kuwa wapiganaji wake walikuwa wamevuka "mstari wa mwisho mwekundu".

Aliwashutumu kwa kushambulia kambi ya kijeshi ya vikosi vya shirikisho tarehe 4 Novemba. TPLF walikanusha kuishambulia kambi.