Bobi Wine apinga matokeo ya uchaguzi nchini Uganda

Muhtasari
  • Bobi Wine anadai uchaguzi wa Alhamisi ulitawaliwa na wizi mbaya zaidi
  • Wine alisema kwamba sasa mapambano yameanza rasmi
  • Wananchi wa Uganda walipiga kura siku ya Alhamisi
aaaaaaaaaaaaa
Bobi Wine aaaaaaaaaaaaa

Mgombea wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amepinga matokeo ya uchaguzi ambayo yametangazwa hadi sasa na kujitaja binafsi kama rais mteuliwa, licha ya tume ya uchaguzi kusema kuwa sio kura zote zilizokwisha hesabiwa.

Bobi Wine anadai uchaguzi wa Alhamisi ulitawaliwa na wizi mbaya zaidi wa kura kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Uganda, lakini hakutoa ushahidi wowote kuhusu madai yake.

Ametangaza kuwa mapambano ndio kwanza yameanza.

 

Bobi Wine, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, anasema kuwa atazungumza na waandishi wa habari tena mnamo saa chache zijazo juu ya kitakachofuatia.

Matokeo ya awali yanayotolewa na Tume ya uchaguzi yanaonesha Rais Yoweri Museveni anaongoza kwa zaidi ya 60%.