Intaneti imerudishwa nchini Uganda baada ya kuzimwa kwa muda wa siku tano.

Muhtasari
  • Intaneti imerudishwa nchini Uganda baada ya kuzimwa kwa muda wa siku tano.
  • Rais Museveni alisema uamuzi, "haiwezekani mtu kuingia Uganda na kuwaamulia kipi kizuri

Intaneti imerudishwa nchini Uganda baada ya kuzimwa kwa muda wa siku tano.

Ingawa mitandao ya kijamii ikiwa bado imefungwa na mtu anaweza kupata mawasiliano hayo kwa kutumia VPN.

Rais Yoweri Museveni aliyeibuka na ushindi katika uchaguzi uliofanyika Januari 14 kwa asilimia zaidi ya 58, aliagiza kufungwa kwa mtandao wa kijamii na hatua hiyo ikachukuliwa usiku wa kabla ya uchaguzi.

 

Hatua hiyo ilichukuliwa muda mfupi baada ya mtandao wa Facebook kufungia mamia ya akaunti za raia wa Uganda wanaoependelea serikali.

Rais Museveni alisema uamuzi, "haiwezekani mtu kuingia Uganda na kuwaamulia kipi kizuri au kibaya".

Awali, akizungumza na kituo cha televisheni cha NBS, Waziri Mkuu Ruhakana Rugunda amesema:

‘’ Mtandao ulikuwa tishio kwa usalama.’’

Waziri Mkuu Rugunda alisema kuwa serikali bado inatathmini kiwango cha tishio hilo kabla ya kuamua kurejesha huduma za mtandao.

Raia wa nchi hiyo ambao wanaegemea upande wa upinanzi ndio waliathirika zaidi kwani walikuwa wa kwanza kuzimiwa mitandao ya kijamii hasa Facebook na Twitter.

Kulingana na Museveni, hakutaka mtu yeyote ambaye sio raia wa Uganda kuingililia shughuli za uchaguzi.