Bobi Wine yuko katika kifungo cha nyumbani, asema hakuna chakula cha mtoto wa jamaa yake

Muhtasari
  • Bobi Wine asema wako katika kifungo cha nyumbani ilhali hawana chakula cha mtoto wa miezi 18
  • KUpitia kwenye ukurasa wake wa twitter alidai kwamba hamna mtu ambaye anaruhusiwa kuingia nyumbani kwake

Mgombea urais aliyeshindwa katika uchaguzi uliokamilika wiki jana Bobi Wine, ametuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kwamba yeye na familia yake "wapo chini ya kifungo cha nyumbani na wamekwama ndani wakiwa na mtoto wa mwaka mmoja unusu".

Wanajeshi wamezunguka nyumba ya mwanasiasa huyo wakidai kuwa anaweza kuchochea wafuasi wake iwapo atatoka nje ya nyumbani hiyo.

Bobi Wine ambaye alikuwa maarufu kama mwanamuziki ameandika katika mtandao wa Twitter kwamba baba ya mtoto huo amezuiwa kutoka nje ya nyumba yake.

 

Pia ameongeza kwamba sasa walipofikia, maziwa ya mtoto yameisha na hawana chakula.

Mwanasiasa huyo, 38, alikuwa mgombea wa urais kwa mara ya kwanza Januari 14 na akapoteza nafasi hiyo kwa Rais Yoweri Museveni, ambaye ameongoza nchi hiyo tangu mwaka 1986.

Bobi Wine anadai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu huku akimshutumu rais kwa madai ya wizi wa kura.

"Siku ya sita tukiwa katika kifungo cha nyumbani , na tuna mtoto wa miezi 18, ambaye alikuwa amekuja kumtembelea shangazi yake(Mke wangu) kabla ya tulivamiwa na kuzingirwa baba yake alikuwa amekatazwa kuja kumuona

Chakula na maziwa yameisha, hamna mtu ambaye anakubaliwa kutoka au kuingia nyumbani kwangu." Bobi Wine Alisema.