Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump aondoka Ikulu

Muhtasari
  • Donald Trump aondoka ikulu kabla ya kuapishwa kwake Joe Biden
Rais anayeondoka wa Marekani Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump ameondoka Ikulu ya Marekani akiwa sambamba na mkewe, Melania Trump.

Wawili hao walielekea kambi ya jeshi, huko Maryland ambapo sherehe za mwisho kuwaaga zilifanyika.

Baada ya shughuli hiyo Rais Trump alisafiri mpaka Florida kwa ndege ya Air Force One, na ataishi katika makazi yake ya kifahari ya la Mar-a-Lago.

 

Akitoa maneno mafupi kwa wanahabari kabla ya kuondoka, Rais Trump amesema Ikulu palikuwa makazi mazuri sana.

''Tumekuwa na miaka minne mizuri sana na tumefanikisha mengi,Tunawapenda Wamarekani na kimekuwa kitu cha kipekee." Alizungumza Trump.

Rais Trump amegusia kuhusu Janga la corona- ambalo lilishika kasi katika kipindi cha miezi tisa iliyopita ya utawala wake.

Vifo vilivyotokana na Covid-19 nchini humo sasa ni zaidi ya 400,000, na idadi ya vifo imeendelea kuongezeka