Trump aponea

Trump aponea:Senate yakosa kumpata hatiani rais wa zamani wa Amerika

Tuna mfumo wa haki nchini na kesi zote dhidi ya marais wa zamani zinaweza kufanyika na mahakama inaweza kumpata yeyote na hatia’ Amesema.

Muhtasari
  •  Baada ya kupatikana bila hatia Trump alitoa taarifa  akilaani mashtaka hayo dhidi yake akisema ni ‘hila kubwa Zaidi katika historia’
  •  Ilikuwa ni mara ya pili kwa senate kufanya kikao cha kumshtaki bwana Trump  ambaye Iwapo hoja hiyo ingepitishwa angezuiwa kabisa kuwahi kugombea tena kiti cha urais .
Mjadala uliopelekea Trump kupatikana bila hatia

 Bunge la seneti la marekani limekosa kuafikia  thuluthi mbili ya maseneta waliohitajika kupigha kura ya kumpata hatiani rais wa zamani Doald Trump kuhusu madai ya uasi dhidi yake kufuatia ghasia na  shambulizi dhidi ya jengo la  Capitol mnamo januari tarehe 6 mwaka huu .

 Maseneta wengi -57 dhidi ya 43 wakiwemo wanachama 7 wa Republican walipiga kura kumueka hatiani Trump lakini idadi hiyo ililemea maseneta 10 kumpata na hatia rais huyo wa zamani hatua inayomaanisha kwamba anaweza kuwania tena urais  .

 Baada ya kupatikana bila hatia Trump alitoa taarifa  akilaani mashtaka hayo dhidi yake akisema ni ‘hila kubwa Zaidi katika historia’

 Ilikuwa ni mara ya pili kwa senate kufanya kikao cha kumshtaki bwana Trump  ambaye Iwapo hoja hiyo ingepitishwa angezuiwa kabisa kuwahi kugombea tena kiti cha urais .

 Baada ya kura hiyo kiongozi mkuu wa  maseneta wa Republican  Mitch McConnell  alisema Trump  alihusika na shambulizi dhidi ya Capitol na kusema hatua hiyo ni ‘utelekezaji mkubwa wa majukumu yake’

 Awali alikuwa amepiga kura kupinga kupatikana na hatia kwa Trump akisema ni ukiukaji wa katiba ka sababu Bwana Trump  sio rais tena . Bwana  McConnell  alihusika pakubwa katika kuchelwesha kikao cha kumhukumu Trump hadialipoondoka afisini januari tarehe 20  .Hata hivyo ameonya kwamba rais huyo wa zamani anaweza kupatikana mashakani na mahakama .

" Hajaepuka lolote kwa sasa .Tuna mfumo wa haki nchini na kesi zote dhidi ya marais wa zamani zinaweza  kufanyika  na mahakama inaweza kumpata yeyote na hatia’  Amesema.