Mwanamfalme Philip amefariki akiwa na miaka 99, Kasri la Buckingham limetangaza

Muhtasari
  • Mwanamfalme Philip, mume wa Malkia Elizabeth II, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99, Kasri la Buckingham limetangaza

Mwanamfalme Philip, mume wa Malkia Elizabeth II, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99, Kasri la Buckingham limetangaza.

Prince Philip alimuoa Mwanamfalme Elizabeth mnamo 1947, miaka mitano kabla ya kuwa Malkia, na alikuwa mwenza wa mfalme ama malkia aliyehudumu kwa muda mrefu katika historia ya Uingereza.

Walikuwa na watoto wanne ,wajukuu wanane na vitukuu 10.

 

Tangazo kutoka Kasri ya Buckingham linaeleza: " Ni kwa masikitiko makubwa, Malkia ametangaza kifo cha mumewe mpenzi, Mwanamfalme Philip, Duke wa Edinburgh.

"Mwanamfalme Philip amefariki kwa amani asubuhi ya leo katika Kasri la Windsor."