Kiongozi wa mapinduzi Mali ajitangaza rais

Muhtasari
  • Kiongozi wa mapinduzi ya Mali ajitangaza rais
  • Rais Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane sasa wameachiwa huru kutoka kizuizi cha kijeshi

Kiongozi wa zamani wa Baraza la jeshi nchini, Kanali Assimi Goïta, amejitangaza kuwa rais wa mpito wa baada ya kuwavua madaraka rais wa mpiti na waziri mkuu wa zamani.

Rais Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane sasa wameachiwa huru kutoka kizuizi cha kijeshi.

Walipelekwa katika kambi ya kijeshi usiku wa Jumatatu katika hatua ambaye iliifanya Mali kukabiliwa na mapinduzi ya pili ya kijeshi ndani ya miezi tisa.

Hatua hiyo ilichochewa na mageuzi katika baraza la mawaziri ambapo maafisa wawili wa jeshi waliohusika na mapinduzi ya awali walipoteza kazi zao.

Kanali Goïta alilalamika kwamba rais aliyeondolewa madarakani hakushauriana naye kuhusu baraza jipya la mawaziri .

Hali ya taharuki imetanda nchi Mali hivi leo lakini kuna utulivu.

Kwa habari nyingine ni kuwa;

Maelfu ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamevuka mpaka na kuingia mji wa Gisenyi nchini Rwanda baada ya mamlaka ya jiji la Goma kutangaza kuondolewa kwa karibu thuluthi tatu ya wakazi wa mji huo, kwa kuhofia uwezekano wa mlima Nyiragongo kulipuka tena.

Wakazi wa Goma na wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa walionekana Alhamisi wakiondoka mji huo kuelekea Gisenyi nchini Rwanda.

Mamlaka nchini Rwanda wanawaelekea za watu hawa katika shule ya sekondari na kituo cha Nkamira ambacho kilikuwa kambi ya zamani ya wakimbizi vilayani Rubavu.

Wale ambao wanaazimia kueleka miji wa mashariki ya Musanze na mji mkuu wa Kigali wanaombwa kuwasilisha cheti cha kuonesha hawana ugonjwa wa Covid-19.