WHO yasikitishwa na madai ya unyanyasaji wa ngono wa wafanyakazi wake dhidi ya raia DRC

Muhtasari
  • WHO yasikitishwa na madai ya unyanyasaji wa ngono wa wafanyakazi wake dhidi ya raia DRC

Shirika la Afya Duniani limesema limesikitishwa na madai ya unyanyasaji wa ngono dhidi unaofanywa na wafanyakazi wake nchini DRC wakati wa mlipuko wa Ebola.

Madai hayo ambayo yalikuja , mwaka mmoja baada ya uchunguzi uliofanywa na shirika la habari za masuala ya kibinadamu na taasisi ya Thomson Reuters.

Wanawake wa eneo hilo walidai kunyweshwa pombe, kuviziwa na kulazimishwa kufanya ngono na wawili walipata ujauzito.

Mkurugenzi wa WHO barani Afrika , Matshidiso Moeti ameomba radhi kwa wanawake na wasichana waliopata masaibu hayo kwa mwaka 2018 na 2020 kwasababu hatua kali zitachukuliwa kwa wafanyakazi hao na watumishi wengine wa afya.

Wachunguzi huru wanasema kuwa mfumo umeshindwa na uzembe wa mtu mmoja katika ripoti yao.

Katibu mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema ripoti hiyo inafadhaisha kuisoma.

Aliomba radhi na kuongeza kuwa hataacha kuahidi kuwasaidia waathirika kwa ulinzi na kupata haki yao.