Wanahabari Maria Ressa na Dmitry Muratov washinda tuzo ya amani ya Nobel 2021

Muhtasari
  • Wanahabari Maria Ressa na Dmitry Muratov washinda tuzo ya amani ya Nobel 2021
Image: BBC

Waandishi wa habari Maria Ressa na Dmitry Muratov wameshinda Tuzo ya Amani ya Nobel kwa "mapambano yao ya ujasiri" kutetea uhuru wa kujieleza huko Ufilipino na Urusi.

Kamati ya Nobel iliwataja wawili hao kuwa "wawakilishi wa waandishi wote wanaotetea msimamo huu".

Washindi wa tuzo hiyo ya kifahari, yenye thamani ya 10m krona za Uswidi (£ 836,000; $ 1.1m), walitangazwa katika Taasisi ya Nobel ya Norway huko Oslo.

Walichaguliwa kati ya wagombea 329.

Wengine waliokuwa wakizingatiwa kwa tuzo hiyo mwaka huu ni pamoja na mwanaharakati wa wa mabadiliko ya tabia nchi Greta Thunberg, kikundi cha haki za vyombo vya habari Reporters Without Borders (RSF) na shirika la afya ulimwenguni (WHO).

Tuzo hiyo hutunukiwa mtu au shirika ambalo "limefanya kazi kubwa zaidi au bora kwa undugu kati ya mataifa".

Mshindi wa mwaka jana alikuwa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu chakula (WFP), ambalo lilituzwa kwa juhudi zake za kupambana na njaa na kuboresha hali ya amani.