Waziri Mkuu Ethiopia awataka raia kuchukua silaha zao kuwadhibiti Waasi

Muhtasari
  • Waziri Mkuu Ethiopia awataka raia kuchukua silaha zao kuwadhibiti Waasi
Abiy Ahmed
Image: BBC

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amewataka raia wa nchi hiyo kubeba silaha zao kwa lengo la kuwazuia waasi kuendelea kudhibiti maeneo mengine ya nchi hiyo.

Ametoa wito huo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook baada ya waasi Kaskazini mwa jimbo la Tigray kuripotiwa kudhibiti miji mingine zaidi, jirani na mkoa wa Amhara.

Mataifa kadhaa ikiwemo Marekani yametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano katika mzozo kwenye eneo hilo uliochukua takribni mwaka mzima na kusababisha hali mbaya ya kibinadamu.

Kundi la Tigray People's Liberation Front (TPLF) limesema linalenga kuzingira na kudhibitie eneo kubwa la mkoa huo wa kaskazini.

Katika taarifa yake siku ya Jumapili, Waziri mkuu Abiy alisema waasi hao wanavyozidi kusonga mbele na kuendelea kudhibiti maeneo mengi kunazidi kuiweka nchi hiyo katika hali hali mbaya.

Amewataka wananchi kujipanga na kuandamana kwa kufuata sheria wakiwa na nguvu na silaha za aina yoyote ili kuwazuia na kuwarudisha nyuma waasi hao na kuzika ugaidi wa kundi la TPL.F