Virusi vipya vya Corona: England yapiga marufuku safari za ndege kutoka mataifa sita ya Afrika

Muhtasari

• Waziri wa afya nchini Uingereza Sajid Javid alisema siku ya Ijumaa kwamba mataifa sita yataongezwa katika orodha , huku baadhi ya ndege zikipigwa marufuku kwa muda.

• Ndege zote kutoka Afrika kusini , Zimbabwe , Botswana, Lesotho na Eswatini zimepigwa marufuku kwa muda kuingia nchini humo.

• Marufuku hiyo ya safari za ndege itasalia hadi mfumo wa kujitenga katika hoteli utakaposhika kasi.

Maafisa wa afya wakipima virusi vya corona
Maafisa wa afya wakipima virusi vya corona
Image: PA MEDIA

Wasafiri wanaowasili nchini England kutoka mataifa tofauti ya Afrika watalazimika kujitenga huku kukiwa na onyo kuhusu aina mpya ya virusi vya corona.

Waziri wa afya nchini Uingereza Sajid Javid alisema siku ya Ijumaa kwamba mataifa sita yataongezwa katika orodha , huku baadhi ya ndege zikipigwa marufuku kwa muda.

Mtaalamu mmoja alitaja virusi hivyo vipya kwa jina B1.1.529, kuwa hatari zaidi kuonekana kufikia sasa na kuna wasiwasi kwamba vina uwezo wa kukwepa kinga.

Hakuna hata kisa kimoja cha virusi hivyo kimeripotiwa nchini Uingereza. Ni wagonjwa 59 pekee waliogunduliwa nchini Afrika Kusini , Hong Kong na Botswana kufikia sasa.

Ndege zote kutoka Afrika kusini , Zimbabwe , Botswana, Lesotho na Eswatini zimepigwa marufuku kwa muda kuingia nchini humo.

Bwana Javid alisema kwamba wanasayansi walikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu virusi hivyo vipya lakini mengi yanahitajika ili watu kujifunza kuvihusu.

Lakini alisema kwamba virusi hivyo vipya vinabadilika mara kadhaa , pengine maradufu ya jinsi virusi vya Delta vinavyojibadilisha.

Aliongezea: Na hilo lina maana kwamba huenda vinaweza kusambaa kwa urahisi na kwamba chanjo tulio nayo kwasasa huenda ni hafifu.

Aliongezea kwamba kuyaongeza mataifa hayo sita katika orodha ya mataifa yaliopigwa marufuku kwa muda ilikuwa hali ya kuchukua tahadhari na hatua ili kujaribu kulinda kwa njia yoyote, mipaka yetu.

Kuanzia saa tisa mchana siku ya Ijumaa raia wasio wa Uingereza pamoja na wale wa kutoka Ireland watapigwa marufuku kuingia England iwapo watakuwa wametoka katika nchi sita katika kipindi cha siku 10 zilizopita.

Raia yeyote wa Ireland au Uingereza anayewasili kutoka mataifa hayo baada ya saa moja siku ya Jumapili atalazimika kujitenga katika hoteli , huku wale wanaorudi kabla ya siku hiyo wakitakiwa kujitenga nyumbani.

Wale ambao wamerudi katika kipindi cha siku 10 wanatakiwa kufanyiwa vipimo vya corona na idara ya afya Uingereza UKHSA

Marufuku hiyo ya safari za ndege itasalia hadi mfumo wa kujitenga katika hoteli utakaposhika kasi.

Marufuku hiyo ya safari za ndege itasalia hadi mfumo wa kujitenga katika hoteli hiyo utakaposhika kasi.