Rwanda yasitisha safari za ndege kuelekea mataifa ya kusini mwa Afrika

Muhtasari
  • Rwanda yasitisha safari za ndege kuelekea mataifa ya kusini mwa Afrika
  • Wale wote wanaohudhuria mikusanyiko kama vile harusi na mazishi lazima wapate chanjo kamili
Image: BBC

Serikali ya Rwanda imetangaza hatua mpya ambazo ni pamoja na kusimamisha safari za ndege kwenda na kutoka nchi za kusini mwa Afrika.

Abiria wote wanaowasili lazima wathibitishe kutokuwa na virusi vya corona na wafanyiwe vipimo vya marudio wanapowasili .

Karantini ya siku saba pia imerejeshwa kwa wasafiri wanaotoka nchi zilizoathiriwa hivi karibuni na mawimbi mapya.

Wale wote wanaohudhuria mikusanyiko kama vile harusi na mazishi lazima wapate chanjo kamili.

Kufuatia maagizo ya serikali kuhusu usafiri, shirika la ndege la Rwandair limesitisha huduma kwenda Afrika Kusini, Zimbabwe na Zambia:

Rwanda ndiyo nchi ya hivi punde zaidi kuweka marufuku ya kusafiri kwenda Afrika Kusini baada ya aina mpya ya virusi vya corona Omicron kugunduliwa nchini humo.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema "amesikitishwa sana" na marufuku dhidi ya nchi yake na mataifa jirani ambapo kirusi hicho kimegunduliwa.

Article share tools

  •  
  •