Mamilioni ya watu wanakufa kutokana na magonjwa sugu ya dawa, ripoti

Muhtasari
  • Mamilioni ya watu wanakufa kutokana na magonjwa sugu ya dawa, ripoti

Zaidi ya watu milioni 1.2 walifariki kote duniani mnamo 2019 kutokana na maambukizo yanayosababishwa na bakteria sugu kwa viua vijasumu, kulingana na utafiti mkubwa zaidi wa suala hilo hadi sasa.

Hii ni zaidi ya idadi ya vifo vya kila mwaka kutokana na malaria au Ukimwi.

Nchi maskini ndizo zimeathirika zaidi lakini ukinzani wa dawa za kuua viini unatishia afya ya kila mtu, ripoti hiyo inasema.

Uwekezaji wa dharura katika dawa mpya na kutumia za sasa kwa busara zaidi unapendekezwa ili kulinda dhidi yake.

Matumizi ya kupita kiasi ya viuavijasumu katika miaka ya hivi karibuni kwa maambukizo madogo-madogo inamaanisha kuwa yanapungua ufanisi dhidi ya maambukizo hatari.

Watu wanafariki kutokana na maambukizi ya kawaida amabyo yalikuwa yakitibika kwasababu ya bakteria ambayo imekuwa sugu kwa matibabu.

Maafisa wa afya wa Uingereza hivi majuzi walionya upinzani dhidi ya viuavijidudu (AMR) ni "janga lililofichwa" ambalo linaweza kuibuka baada ya Covid-19 isipokuwa dawa za kuua viua vijasumu hazitaidhinishwa.

Makadirio ya vifo vya kimataifa kutoka kwa AMR, iliyochapishwa katika Lancet, yanatokana na uchambuzi wa nchi 204 na timu ya watafiti wa kimataifa, wakiongozwa na Chuo Kikuu cha Washington, Marekani.