Urusi na Ukraine: Ukraine inafanya kila liwezekanalo kuwanusuru wapiganaji waliosalia Mariupol

Muhtasari

• Ukraine inafanya ‘’kila liwezekanalo na lisilowezekana ’’ kuwanusuru wapiganaji wengine waliobaki ambao wamekwama katika kiwanda cha chuma kilichopo Mariupol.

Takriban mabasi mengine saba yalionekana yakiondoka kutoka kwenye eneo la Azovstal Jumanne na baadaye kuwasili katika kijiji kinacpodhibitiwa na wasi wanaoungwa mkono na Urusi, limeripoti Shirika la habari la Reuters.
Takriban mabasi mengine saba yalionekana yakiondoka kutoka kwenye eneo la Azovstal Jumanne na baadaye kuwasili katika kijiji kinacpodhibitiwa na wasi wanaoungwa mkono na Urusi, limeripoti Shirika la habari la Reuters.
Image: Reuters

Ukraine inafanya ‘’kila liwezekanalo na lisilowezekana ’’ kuwanusuru wapiganaji wengine waliobaki ambao wamekwama katika kiwanda cha chuma kilichopo Mariupol, amesema afisa wa ngazi ya juu.

Naibu Waziri wa ulinzi Hanna Maliar amesema kuwa kyiv inafahamu ni wanajeshi wake wangapi ambao bado wamekwama katika kiwanda hicho, lakini akasisitiza kwamba hiyo ni ‘’taarifa ya siri’’.

Jumatatu, wapiganaji 264-wengi wao wakiwa wameumia vibaya-waliokolewa na kupelekwa katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.

Jumanne, mabasi mengine saba, yalionekana yakiondoka katika eneo hilo, limesema shirika la habari la Reuters.

Iliongeza kuwa msafara huo baadaye uliwasili katika kijiji cha Olenivka, kilichotekwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi kilichopo katika jimbo la mashariki la Donbas.