Wanawake wapigwa marufuku kuonyesha nyuso zao kwenye TV Afghanistan

Muhtasari

•Uamuzi huo unakuja wiki mbili baada ya wanawake wote kuamriwa kuficha nyuso zao wakiwa hadharani, au vinginevyo kupewa adhabu.

Watangazaji wanawake Afghanistan wanapaswa kuvaa vazi la namna hii wakiwa wanatangaza
Watangazaji wanawake Afghanistan wanapaswa kuvaa vazi la namna hii wakiwa wanatangaza
Image: BBC

Kundi la Taliban limewaamuru watangazaji wa televisheni wa kike wa Afghanistan na wanawake wengine kwenye kufunika nyuso zao wakiwa hewani kwenye vipindi vyaTelevisheni.

Vyombo vya habari viliambiwa kuhusu agizo hilo siku ya Jumatano, msemaji wa polisi wa kidini aliambia BBC. Uamuzi huo unakuja wiki mbili baada ya wanawake wote kuamriwa kuficha nyuso zao wakiwa hadharani, au vinginevyo kupewa adhabu.

Vikwazo vinaimarishwa dhidi ya wanawake - wakipigwa marufuku kusafiri bila kuambatana na mwanaume na wasichana marufku kuhudhuria masomo katika shule za sekondafri.

Getty ImagesCopyright: Getty ImagesWatangazaji wanawake Afghanistan wanapaswa kuvaa vazi la namna hii wakiwa wanatangazaImage caption: Watangazaji wanawake Afghanistan wanapaswa kuvaa vazi la namna hii wakiwa wanatangaza

Mwanahabari mmoja wa kike wa Afghanistan anayefanya kazi katika kituo cha televisheni cha mjini Kabul, ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema alishtuka kusikia taarifa hiyo. "Wanatuwekea shinikizo zisizo za moja kwa moja kutuzuia kutangaza kwenye TV," aliambia BBC. "Ninawezaje kusoma habari nikiwa nimeziba mdomo? Sijui la kufanya sasa - lazima nifanye kazi, mimi ndiye mlezi wa familia yangu."

Amri hiyo mpya itaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 21 Mei, shirika la habari la Reuters liliripoti, likimnukuu msemaji wa Wizara ya Taliban ya Kuzuia Umakamu na Kukuza Utu wema.