Mamia ya miili yapatikana kwenye vifusi Mariupol

Muhtasari

• Mamia ya miili imepatikana kwenye vifusi vya majengo yaliyoharibiwa huko Mariupol, kulingana na mshauri wa meya wa jiji hilo.

Majengo yaliyoharibiwa huko Mariupol yanaondolewa na Warusi wanaokalia eneo
Majengo yaliyoharibiwa huko Mariupol yanaondolewa na Warusi wanaokalia eneo
Image: EPA

Mamia ya miili imepatikana kwenye vifusi vya majengo yaliyoharibiwa huko Mariupol, kulingana na mshauri wa meya wa jiji hilo.

Petro Andryushchenko alizungumza kwenye ujumbe wa Telegramu kuhusu ‘’msafara usioisha wa vifo’’ katika jiji la bandari linalokaliwa, ambapo miili kati ya 50 na 100 kwa kila eneo la orofa inachukuliwa kutoka chini ya vifusi na kusafirishwa hadi kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti au - kulingana na mahali miili hiyo iko. - kutupa taka.

Katika chapisho hilo, lililochapishwa jana, alisema majengo takriban thuluthi mbili yamekaguliwa na wanajeshi waliovamia hadi sasa.

Mwezi uliopita, mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Donetsk kama inavyojiita alisema kuwa 60% ya majengo huko Mariupol yameharibiwa, ambayo 20% yao hayawezi kujengwa tena.

Lakini katika chapisho la kufuatilia asubuhi ya leo, Andryuschenko anasema utafutaji katika wilaya ya Ukingo wa Kushoto imesitishwa, akisema: ‘’Wavamizi hatimaye wameanza kubomoa majumba na kukataa kutafuta miili ya waliouawa chini ya vifusi.’’

Anasema haijajulikana kamwe ni wakazi wangapi wa Mariupol walikufa na bado wako chini ya vifusi - na watazikwa pamoja na takataka.

‘’Hakuna maneno. Hasira tu,’’ anasema.