Mahakama yaamuru mtoto aondolewe mashine ya kupumua 'afe'

Muhtasari

•Archie Battersbee, 12, alikutwa amepoteza fahamu nyumbani kwao Southend, Kusini Mashariki mwa Uingereza, Aprili 7.

•Mahakama ya Uingereza imeatoa hukumu kuthibitisha kwamba Archie Battersbee amefariki na lazima aondolewe mashine ya msaada wa maisha

Image: BBC

Matibabu ya mtoto mmoja wa kiume huko Uingereza ambaye alipoteza fahamu kutokana na majeraha ya ubongo yanapaswa kusitishwa, hakimu wa mahakama ya Uingereza ametoa uamuzi huo katika kesi inayozua utata nchini humo.

Archie Battersbee, 12, alikutwa amepoteza fahamu nyumbani kwao Southend, Kusini Mashariki mwa Uingereza, Aprili 7.

Madaktari wanaomtibu katika Hospitali ya Royal London katika mji mkuu wa Uingereza waliambia mahakama kwamba mvulana huyo "ana uwezekano mkubwa" "ubongo wake umekufa" kwa maana hautafanya kazi tena na wakaomba aondolewe mashine maalumu ya uhai inayomsaidia kupumua.

Mama yake Archie, Hollie Dance, amesema "amesikitishwa" na uamuzi huo. Familia inapanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Archie alipata shida ya ubongo na upoteza wakati wa tukio moja nyumbani kwake, ambalo mama yake anaamini huenda lilihusiana na ushindani wa kujifurahisha wa mtandaoni.

Tangu wakati huo, hajapata fahamu tena.

Kutofautina na Hospitali

Wazazi wa Archie hapo awali hawakukubaliana na uamuzi wa hospitali, na wamepata usaidizi wa kisheria kutoka Shirika moja la Kikristo linaitwa Christian Legal Center Kikristo.

"Nimesikitishwa na kusikitishwa sana na uamuzi wa hakimu baada ya kupigana vita vya kisheria kwa wiki kadhaa, wakati nilichotaka ni kuwa kando ya mtoto wangu," mama ya Archie alisema katika taarifa iliyotolewa baada ya kupata habari kuhusu uamuzi wa mahakama. 

Mama ya Archie anasema kwamba hatakata tamaa.
Mama ya Archie anasema kwamba hatakata tamaa.
Image: HOLLY DANCE

"Kutoa hukumu hii kupitia matokeo ya kipimo cha MRI kwamba 'pengine' atakufa hiyo haitoshi. Hii itakuwa ni mara ya kwanza mtu kutangazwa 'pengine' amekufa kwa mujibu wa kipimo cha MRI."

Alisema alihisi "kuchukizwa" kwamba hospitali na hakimu hawakuzingatia matakwa ya familia, na kuongeza kwamba hadhani kwamba "Archie alipewa muda wa kutosha."

"Moyo wake bado unadunda, amenishika mkono na kama mama yake najua bado yuko hai," alisema.

"Hadi kwa mapenzi ya Mungu, vinginevyo sitakubli kumuacha. Najua miujiza ipo ambapo watu wamepona kutoka tatizo la ubongo kufaau kutofanya kazi".

"Tunakusudia kukata rufaa na hatutakata tamaa kwa Archie." Mawakili wanaowakilisha hospitali hiyo walikuwa wamemtaka jaji kuamua ni hatua gani ingemfaa Archie.

Wakati wa siku tatu za kusikilizwa kwa kesi hiyo katika Kitengo cha Familia cha mahakama hiyo wiki iliyopita, wataalamu walihakikisha kwamba vipimo tofauti vilivyofanywa kwa mvulana huyo havijaonyesha shughuli za ubongo "zinazoonekana".

"Haiwezekani kurejeshwa"

Katika uamuzi uliotolewa, Jaji Arbuthnot alihitimisha kwamba Archie alikufa saa sita mchana wa Mei 31, kulingana na picha za MRI za siku hiyo.

Image: HOLLIE DANCE

Mahakama ya Uingereza imeatoa hukumu kuthibitisha kwamba Archie Battersbee amefariki na lazima aondolewe mashine ya msaada wa maisha

Jaji anaona kuwa imethibitishwa kuwa ubongo wa kijana huyo haufanyi kazi.

"Ninatoa ruhusa kwa wataalamu wa matibabu katika Hospitali ya Royal London kusitisha zoezi la kumsaidia kwa mashine ya upumuaji Archie Battersbee."

Hakimu pia alibaini pia kwamba namna familia ya Archie ilivyhoamua kujitoa ni jambo kubwa la "ajabu".

"Ikiwa Archie atabaki kwenye mashine za hewa, matokeo yake ni kifo cha ghafla, na matarajio ya kupona hayapo," alisema. "Hawezi kufurahia maisha na kutofanya kazi kwa ubongo wake hakuwezi kurekebishwa. Hawezi kupona ama kupata nafuu. Ubaya wa kifo cha ghafla kama hicho ni kutoweza kwa familia yake kipenzi kumuaga."

Jaji alisema kwamba kama hangehitimisha kwamba Archie alikuwa amekufa, angetoa uamuzi kwamba haikuwa vyema kuendelea kupokea matibabu ya kumudu maisha. "Hatua nilizozichukua hapo juu ni halali," aliongeza.

Alistair Chesser, mkurugenzi wa matibabu wa Barts Health NHS Trust, taasisi inayoendesha hospitali hiyo, alisema "Masikitiko na majonzi" yake zilikuwa kwa familia ya Archie.

"Kwa mujibu wa miongozo iliyotolewa na mahakama, madaktari wetu watatoa huduma bora zaidi huku mashine ya msaada wa maisha ikiondolewa," Chesser alisema.

Hata hivyo, kabla ya kuanza mchakato wowote, wataipatia familia muda iwapo wataamua kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo