Mwanaume achoma kaburi la mama mkwe wake kwa hasira

Muhtasari

•Mwanamume huyo alimwaga petroli kwenye kaburi hilo mnamo Mei 13, na kutishia kutuma picha za eneo hilo kwa mke wake wa zamani.

•Polisi wanasema kuwa kesi hiyo inachunguzwa na mwanamume huyo amekamatwa baada ya msako uliodumu kwa saa 24.

Image: AFP

Mwanaume mmoja raia wa Pakistani ameripotiwa kuchoma moto kaburi la mama mkwe wake aliyefariki miaka 25 iliyopita huko Layyah, jimbo la Punjab.

Mwanamume huyo ambaye hakutajwa jina alimwaga petroli kwenye kaburi hilo mnamo Mei 13, na kutishia kutuma picha za eneo hilo kwa mke wake wa zamani.

Suala hilo lilikuja baada ya mke wake wa zamani, ambaye alitalakiana naye miaka 10 iliyopita, kujitolea kuolewa tena, jambo ambalo alikataa.

Shemeji yake ambaye alifungua kesi hiyo alisema mwanamume huyo alitishia kuchoma kaburi la mamake baada ya kukasirishwa na kukataliwa na dadake.

Msemaji wa polisi amesema kaburi hilo limepatikana likiwa na dalili za kuchomwa moto, na mtu huyo amekamatwa na atafikishwa mahakamani.

Katika ujumbe wake aliotishia kuchoma moto kaburi la mama yake Polisi walisema baada ya kupata taarifa hizo walikwenda eneo la tukio na kuwahoji wanafamilia wa binti huyo na wakazi.

Kisha wakafanya kazi ya kumtafuta na kumkamata mhusika.

Polisi wanasema kuwa kesi hiyo inachunguzwa na mwanamume huyo amekamatwa baada ya msako uliodumu kwa saa 24 na atafikishwa mahakamani.

Alipotafutwa na BBC, kaka ya mwanamke mwathirika anasema kuwa mwanamume huyo alikuwa amejitolea kumuoa tena dada yake, lakini baada ya kukataliwa mara kadhaa, mwanamume huyo alikasirika na kuchoma kaburi la mama yake.

“Baada ya muda nilipata ujumbe kwenye mtandao wa WhatsApp kutoka kwenye simu ya dada yangu ikiwa na picha za kaburi la mama likiwashwa kwa gesi.’’

alisema alienda kaburini na familia yake na kuuzima moto huo na kutoa taarifa kwa polisi. Familia ilisema haikutaka kuzungumzia suala hilo kwa wakati huu.

“Mumuadhibu tu mshtakiwa, tunaomba hilo.” Kufuatia kukamatwa kwa mtu huyo, polisi wa Punjab walitangaza kukamatwa kwake kupitia mtandao wa Twitter. Watu wengi walijibu kwa hasira.