Mzozo wa Rwanda na DR Congo: Marais watarajiwa kufanya mazungumzo

Wiki mbili zilizopita viongozi wa Afrika Mashariki waliidhinisha kuundwa kwa kikosi cha kijeshi cili kumaliza machafuko mashariki mwa DR Congo.

Muhtasari

• Rais wa Rwanda, Paul Kagame, jana ametoa wito wa kutatuliwa kwa mgogoro wa kisiasa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi, anatazamiwa kukutana na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame kwa mazungumzo katika mji mkuu wa Angola, Luanda, wiki hii kujaribu kusuluhisha mzozo wa mashariki mwa DR Congo.

Ofisi ya rais wa Angola ilisema mazungumzo hayo yatafanyika siku ya Jumatano.

Kumekuwa na hofu ya kuzuka upya kwa shughuli za waasi na kuzidisha mvutano kati ya DR Congo na Rwanda.

Kinshasa inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, jana ametoa wito wa kutatuliwa kwa mgogoro wa kisiasa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika mahojiano na shirika la utangazaji la serikali, alisema uhasama uliopo hauwezi kutatuliwa kwa nguvu pekee.

Wiki mbili zilizopita viongozi wa Afrika Mashariki waliidhinisha kuundwa kwa kikosi cha kijeshi cili kumaliza machafuko mashariki mwa DR Congo.