Waziri Mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe amefariki-vyombo vya habari vya Japan

Mshambulizi anayeshukiwa - aliripotiwa kuwa mwanamume mwenye umri wa miaka 40

Muhtasari
  • Abe, 67, ambaye anasalia kuwa waziri mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi nchini Japan, alipigwa risasi alipokuwa akitoa hotuba ya kampeni

Waziri Mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe amefariki, kwa mujibu wa shirika la habari la  kitaifa la Japan.

Abe, 67, ambaye anasalia kuwa waziri mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi nchini Japan, alipigwa risasi alipokuwa akitoa hotuba ya kampeni.

Mshambulizi anayeshukiwa - aliripotiwa kuwa mwanamume mwenye umri wa miaka 40 - alikabiliwa katika eneo la  tukio na kukamatwa.

Bw Abe alipigwa risasi mara mbili alipokuwa akitoa hotuba katika mji wa kusini wa Nara siku ya Ijumaa asubuhi.

Mara moja alianguka na kukimbizwa katika hospitali ya karibu. Picha zilizopigwa eneo la tukio zilimuonyesha akivuja damu. Maafisa wa usalama katika eneo la tukio walimkabili mshambuliaji huyo, na mshukiwa mwenye umri wa miaka 41 sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi.