Polisi wa Nigeria wagundua miili 20 katika eneo linaloshukiwa kuwa 'takatifu'

Polisi wamewakamata watu watatu kuhusiana na miili hiyo iliyokaushwa.

Muhtasari

•Polisi wamewakamata watu watatu kufuatia ugunduzi wa miili 20 iliyokaushwa karibu na mji wa Benin katika jimbo la Edo.

Polisi wamewakamata watu watatu kuhusiana na miili iliyokaushwa
Polisi wamewakamata watu watatu kuhusiana na miili iliyokaushwa
Image: BBC

Polisi kusini mwa Nigeria wamewakamata watu watatu kufuatia ugunduzi wa miili 20 iliyokaushwa karibu na mji wa Benin katika jimbo la Edo.

Miili hiyo ilipatikana katika jengo linaloshukiwa kutumiwa kama kaburi la voodoo.

Msemaji wa polisi, Chidi Nwabuzor, ameiambia BBC kwamba maiti 15 za wanaume, wanawake watatu na watoto wawili zimegundulika.

Haijawa wazi ni kwa muda gani zimekuwa pale.

Aliongeza kuwa maafisa wa polisi wenye silaha na walinzi wa eneo walikuwa wamevamia jengo hilo lililopo nje tu ya mji kufuatia taarifa waliyopewa kwa siri.

Ugunduzi wa miili hiyo umewashitua watu nchini Nigeria na wakazi wa eneo hilo wanasema wametishwa na tukio hilo.

Wengi wanauliza ni kwa vipi miili hiyo iliweza kufichwa pale bila majirani kufahamu.