Korea Kusini: Watu 154 wafariki katika mkanyaganyo wa sherehe za Halloween

Rais Yoon Suk-yeol ametangaza kipindi cha maombolezo ya kitaifa

Muhtasari

• Raia 20 wa kigeni ni miongoni mwa waliofariki.

Walionusurika walisema walitatizika kupumua huku miili ikitapakaa juu ya mingine baada ya mkasa huo .

154 Wafariki katika mkanyaganyo sherehe za halloween, Korea Kusini
154 Wafariki katika mkanyaganyo sherehe za halloween, Korea Kusini
Image: BBC NEWS

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol ametangaza kipindi cha maombolezo ya kitaifa kufuatia mauaji ya watu 153 katika mkanyagano wa sherehe za halloween uliotokea Jumamosi usiku na kuwajeruhi wengine 82 huko Seoul.

Kipindi cha maombolezo kitaendelea hadi msukosuko wa maafa utakapodhibitiwa, Yoon aliwaambia raia wa Korea Kusini kutoka ofisi ya rais.

"Moyo wangu ni mzito na ninajitahidi kukabiliana na huzuni yangu," alisema, akiongeza kuwa alihisi "kuwajibika kwa maisha na usalama wa watu".

Maafisa sasa wanaagizwa kufanya ukaguzi wa dharura wa sherehe zote za Halloween na sherehe zingine za ndani.

Kufuatia hotuba hiyo, Yoon alitembelea eneo la mkasa ambapo mkanyagano ulisababisha maafa hayo .

Ni nini kilifanyika huko Seoul?

Ikiwa unajiunga nasi tu, kuna mkasa mkubwa uliotokea jana Jumamosi Seoul,Korea Kusini ambapo mkanyagano wa watu katika sherehe za halloween ulisababisha vifo vya watu 153 na wengine 82 kujeruhiwa .

Haya ndio mengine zaidi tunayojua hadi sasa

-Raia 20 wa kigeni ni miongoni mwa waliofariki, huduma za dharura zilisema

-Ilitokea wakati umati mkubwa wa watu waliosherehekea Halloween ulipoingia kwenye kichochoro chembamba katika eneo maarufu la Itaewon.

-Wengi wa waliouawa walikuwa katika ujana wao miaka ya 20 , maafisa wanasema

-Walioshuhudia waliripoti polisi wakijitahidi kudhibiti umati wa watu waliokuwa wakisherehekea

-Walionusurika walisema walitatizika kupumua huku miili ikitapakaa juu ya mingine baada ya mkasa huo .

-Ilikuwa tukio la kwanza la Halloween huko Seoul tangu masharti ya Covid ikiwemo kuvaa barakoa kutokaribiana kuondolewa

-Rais wa Korea Kusini, Yoon Suk-yeol ametembelea wilaya ambayo tukio hilo lilitokea na kuagiza uchunguzi ufanyike na kikosi kazi kusaidia majeruhi.