Mtoto wa mwaka mmoja auawa na mbwa nchini Afrika Kusini

Hili ni shambulio la tatu chini ya kipindi cha wiki moja, tovuti ya habari ya IOL inaripoti.

Muhtasari
  • Kumekuwa na hasira ya umma kuhusu ripoti za mbwa kushambulia na kuua watoto katika wiki za hivi karibuni

Mtoto wa mwaka mmoja ameumwa na mbwa aina ya pit bull hadi kufa katika jimbo la Eastern Cape nchini Afrika Kusini, kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini humo.

Mazingira ya shambulio hilo bado hayajabainika lakini mbwa huyo anaaminika kuwa wa jirani, shirika la utangazaji la SABC linaripoti.

Mtoto huyo alikimbizwa katika kituo cha afya lakini alifariki wakati matabibu walipokuwa wakimhudumia, mtangazaji huyo alisema.

Hili ni shambulio la tatu chini ya kipindi cha wiki moja, tovuti ya habari ya IOL inaripoti.

Kumekuwa na hasira ya umma kuhusu ripoti za mbwa kushambulia na kuua watoto katika wiki za hivi karibuni.