Majambazi wavamia kanisa katoliki na kuchoma kasisi hadi kufa

Waliingia na kuanza kufyatua risasi na walipomkosa kasisi huyo, wakatia jengo zima moto na kusimama hapo hadi likateketea lote kasisi akiwa ndani.

Muhtasari

• Majambazi hao walidaiwa kuvamia kanisa hilo majira ya saa saba asubuhi na kuanza kufyatua risasi za hapa na pale kiholela.

Picha ya kanisa likichomeka
Picha ya kanisa likichomeka
Image: Hisani

Majambazi wanaokiziwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram wameripotiwa kuvamia kanisa moja ya Kikatoliki asubuhi ya Jumapili nchini Niger na kumuua kasisi wa kanisa hilo kwa kumchoma moto.

Kulingana na jarida la nchi jirani ya Nigeria, majambazi hao walivamia kanisa hilo lililopo katika Jumuiya ya Kafin Koro katika eneo la Serikali ya Mtaa wa Paikoro Niger ambapo Padre Isaac Achi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro na Paulo alikuwa akiandaa misa kabla ya kumteketeza.

Majambazi hao walidaiwa kuvamia kanisa hilo majira ya saa saba asubuhi na kuanza kufyatua risasi za hapa na pale kiholela wakati wakielekea kwenye makazi ya kasisi huyo.

“Kwa mujibu wa mkazi wa jamii hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Paul, majambazi hao walijigawanya katika makundi mawili huku wengine wakienda katika makazi rasmi ya kasisi huyo wa Kanisa Katoliki, wengine walisalia katika mji huo wakifyatua risasi ili kuepuka aina yoyote ya uingiliaji kati,” jarida hilo liliripoti.

Shuhuda huyo alisema kwamba wakati majambazi hao walishindwa kumfikia marehemu kasisi huyo kwa haraka kutokana na vyumba vingi vya kuchanganya katika makazi yake, walichoma jengo hilo zima na kungoja hadi likaungua na kuwa majivu kasisi akiwa ndani.

Uvamizi wa aina hiyo si mara ya kwqanza kuripotiwa katika mataifa ya ukanda wa Afrika Magharibi ambapo wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wakiwashambulia watu haswa wakilengac zaidi Wakristu.

Kwa muda mrefu, kundi hilo la wanamgambo limekuwa likiendeleza mashambulizi na utekaji nyara katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria, wakidai kupewa uhuru wa kutawala eneo hilo ambalo wenyeji wengi ni Waislam.