Watu 4 wafariki, kadhaa wajeruhiwa baada ya gari la mashindano kuwagonga watazamaji

Ambulensi kadhaa na helikopta za uokoaji zilitumwa kwenye eneo la tukio, na mkutano huo ulisitishwa mara moja.

Muhtasari
  • Video kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha gari likipoteza mwelekeo wenye barabara ya lami kabla ya kuteleza na kuwaingia watazamaji waliokuwa wamekusanyika kutazama mbio hizo.
Safari Rally
Image: Hisani

Watu wanne waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa siku ya Jumapili wakati dereva aliyekuwa akishiriki katika mashindano ya magari yawa Hungary Motorsport alipotoka barabarani na kuwagonga watazamaji.

Kulingana na taarifa ya polisi, bado haijabainika ni kwa nini gari lililokuwa likishiriki katika Mashindano ya siku mbili ya Esztergom Nyerges katika eneo la kaskazini mwa Hungary liliacha njia yake.

Ajali hiyo ilitokea kati ya miji ya Labatlan na Bajot kaskazini mwa kaunti ya Komarom Esztergom, na kuacha takriban watu 4 wakiwa wamekufa na saba kujeruhiwa, Polisi walisema na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea.

Ambulensi kadhaa na helikopta za uokoaji zilitumwa kwenye eneo la tukio, na mashindano hayo ulisitishwa mara moja.

Video kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha gari likipoteza mwelekeo kwenye barabara ya lami kabla ya kuteleza na kuwagonga watazamaji waliokuwa wamekusanyika kutazama mbio hizo. 

Chama cha Kitaifa cha Michezo cha Hungary (MNASZ) kilitoa rambirambi kwa jamaa na wanafamilia wa wahasiriwa.

Iliapa kushirikiana na mamlaka kuchunguza mazingira ya ajali hiyo bila kuchelewa.