Sifanyi uchekeshaji wowote, mapenzi yangu yako kwa mbio za safari rally - Arap Marindich

Alisema kuwa anapanga kushiriki katika mbo za magari wakati mmoja lakini akasema kuwa inahitaji mazoezi sana, "Rally si kitu rahisi. Unaeza roll ukianza tu na uende,”

Muhtasari

• Alisema kuwa kwa vile mapenzi yake yanalenga sana katika mbio za magari, wao huwa hawaonekana sana.

• “Sasa ni mpaka mwaka kesho tena, isipokuwa kitu kitokee tu hapa kati lakini si ile ya ucheshi,” aliweka wazi.

Arap Marindich azungumza kwa nini hazungumziwi sana.
Arap Marindich azungumza kwa nini hazungumziwi sana.
Image: Facebook

Dereva wa matatu aliyegonga vichwa vya habari kutokana na picha zake kutumiwa kama vichekesho yaani meme, Arap Marindich amevunja ukimya kuhusu kile anakifanya baada ya umaarufu huo wa ghafla.

Katika mazungumzo kwa njia ya simu ya mwandishi wa tovuti ya Radio Jambo, Marindich alisema kuwa wengi wanahisi amepotea lakini hawafahamu kwamba yeye hakuanza kama mchekeshaji bali alijulikana tu kutokana na mapenzi yake kwenye mbio za magari ya safari Rally.

“Ilitokea kwamba sisi tulikuwa sana si katika uchekeshaji bali katika mbio za magari ya safari rally. Yetu sisi hatufanyi ucheshi wowote, tuko tu kwa rally. Hata Naivasha tulienda kama mabalozi wa benki ya KCB,” alisema meneja wake.

Alisema kuwa kwa vile mapenzi yake yanalenga sana katika mbio za magari, wao huwa hawaonekana sana, huku akisema kuwa tena watazama mpaka mwaka kesho katika mbio za magari, isipokuwa kitu kingine kama hicho kitokee tena hapa katikati.

“Sasa ni mpaka mwaka kesho tena, isipokuwa kitu kitokee tu hapa kati lakini si ile ya ucheshi,” aliweka wazi.

Alisema kuwa anafikiria katika kujaribu pia wakati mmoja kujiunga katika mbio hizo za magari, lakini akasema kuwa inahitaji ajifunze sana kwa kile alisema kuwa mbio za magari si kama udereva mwingine wa kukurupukiwa tu.

“Marindich ashawahi kuendesha lakini si ile ya mashindano ya mbio, hapana. Tunapanga lakini unajua hiyo lazima uingie mazoezi vizuri na rally si kitu rahisi. Unaeza roll ukianza tu na uende,” alisema.