Hatima ya tamasha la 'kwanza na kubwa zaidi' la ngono nchini Korea

Lee Hee Tae alitarajia mashabiki 5,000 wangemiminika kuona waigizaji wa filamu za ponografia wa Kijapani wanaowapenda.

Muhtasari

• Tamasha hilo lilifutiliwa mbali zikiwa zimesalia saa 24.

• Mwezi mmoja kabla, vikundi vya kutetea haki za wanawake kutoka mji wa Suwon, ambako tukio hilo lilipaswa kufanyika, walijitokeza kupinga.

Image: BBC

Lee Hee Tae alikuwa na matumaini makubwa kwa tamasha lake la ngono, ambalo aliliita kwa fahari kama "La kwanza na kubwa zaidi" nchini Korea Kusini.

Alitarajia mashabiki 5,000 wangemiminika kuona waigizaji wa filamu za ponografia wa Kijapani wanaowapenda, ambao walikuwa wakisafirishwa kwa ndege kwa ajili ya tukio la wikendi iliyopita. Kulikuwa na maonyesho ya mitindo.

Lakini zikiwa zimesalia saa 24 tu, tamasha hilo lilifutiliwa mbali.

Korea Kusini inajulikana kwa mtazamo wake wa kihafidhina wa ngono na burudani ya watu wazima. Utupu wa hadharani na maonyesho ya aina hiyo yamepigwa marufuku, na ni kinyume cha sheria kuuza au kusambaza filamu za watu wazima ingawa sio marufuku kuzitumia.

"Takriban kila nchi iliyoendelea huwa na tamasha la ngono, lakini hapa Korea Kusini hatuna hata utamaduni wa burudani ya watu wazima. Nataka kuchukua hatua za kwanza za kuunda moja," alisema Lee Hee Tae, ambaye kampuni yake ya Play Joker iliunda filamu kama hizo zisizo na makali -kabla ya kuanza kupanga hafla na shughuli zinazohusiana na aina hiyo ya burudani .

Mwezi mmoja kabla, vikundi vya kutetea haki za wanawake kutoka mji wa Suwon, ambako tukio hilo lilipaswa kufanyika, walijitokeza kupinga. Walishutumu tamasha hilo kwa kuwatumia vibaya wanawake katika nchi ambayo unyanyasaji wa kijinsia umeenea.

Walibishana kwamba hii haikuwa tamasha iliyolenga jinsia zote mbili. Maonesho ya wanawake waliovalia mavazi duni ulipendekeza walio na tikiti wanaweza kuwa wanaume kwa wingi.

Meya wa eneo hilo alilaani tukio hilo kwa kufanyika karibu na shule ya msingi na mamlaka ilitishia kunyang'anya leseni ya ukumbi huo ikiwa itaendelea. Ukumbi baadaye ulikataa kuwa mwenyeji .

Akiwa amechanganyikiwa, lakini bila kufadhaika, Bw Lee alibadilisha maeneo, lakini msururu wa matukio sawa ulijitokeza. Mamlaka hiyo mpya ilishutumu tamasha hilo kwa "kuweka mtazamo potovu wa ngono" na kusisitiza kuwa ukumbi huo ughairi. Kisha, Bw Lee alipata meli iliyotiwa nanga kwenye mto huko Seoul. Lakini, kufuatia shinikizo kutoka kwa baraza hilo, mkodishaji wa boti hiyo alitishia kuizuia na kukata umeme ikiwa promota wake ataruhusu tamasha hilo kuendelea.

Katika kila upande, Bw Lee alilazimika kupunguza tamasha huku wenye tikiti wakiitisha kurejeshewa hela zao, na kumgharimu mamia ya maelfu ya pauni.

Sehemu ya bango la tamasha hilo 2024
Sehemu ya bango la tamasha hilo 2024

Akiwa hana chaguo jingine, alipata baa ndogo ya chini ya ardhi katika kitongoji cha Gangnam huko Seoul, ambayo inaweza kubeba karibu watu 400. Wakati huu aliweka eneo hilo siri.

Kwa hivyo, baraza la Gangnam liliandikia kila moja ya mamia ya mikahawa yake likiwaonya kuwa litafungwa ikiwa wataandaa tamasha hilo, likishutumu kuwa "linaeneza madhara kwa maadili". Lakini baa ilisimama kidete.

Kisha, siku moja kabla, nyota wa filamu za watu wazima kutoka Japan waliojiondoa. Shirika lao lilisema msukosuko kwenye tamasha "umefikia kiwango cha juu" na wanawake walikuwa na wasiwasi wanaweza kushambuliwa na hata kuchomwa visu.

Kutoka ofisini kwake Gangnam, Bw Lee aliambia BBC kwamba alishtushwa na matukio ambayo yalikuwa yamefanyika kwa "njia isiyoweza kufikirika", akiongeza kwamba alipokea vitisho vya kuuawa. "Nimechukuliwa kama mhalifu bila kufanya chochote kinyume cha sheria", alisema, na kusema kuwa tamasha hilo halikuvunja sheria .

Play Joker iliandaa hafla zenye kuvutia hapo awali. Mwaka jana walifanya gwaride la wanawake katika mitaa ya Seoul aakiwa amevalia karatasi za kadibodi, akiwaalika wapita njia kuweka mikono yao ndani na kugusa matiti yake.

Bw Lee anasema anataka kupinga mitazamo ya Korea kuhusu ngono na ponografia, ambayo imesalia kuwa ya zama za kale.

"Mamlaka ni wanafiki. Ukiingia mtandaoni kila mtu anashiriki ponografia, basi watu wanatoka na kujifanya hawana hatia. Je, tutaendelea na udanganyifu huu hadi lini?"

Ingawa tovuti maarufu za kimataifa za ponografia haziwezi kufikiwa kutoka Korea Kusini, wengi wanajua jinsi ya kutumia VPN za mtandao kubatilisha vikwazo.

Bw Lee alifanya tukio kama hilo mwaka jana ambalo halikutangazwa sana.
Bw Lee alifanya tukio kama hilo mwaka jana ambalo halikutangazwa sana.

Kundi ambalo lilipinga tukio la awali, Suwon Women's hotline lilielezea kufutwa kwa tamasha hilo kama "ushindi". "Chochote waandaaji wanasema, hii haikuwa sherehe ya ngono, lakini ukandamizaji na unyanyasaji wa wanawake, na tasnia ya ngono inahimiza unyanyasaji dhidi ya wanawake," alisema Go Eun-chae, mkurugenzi wa shirika linalotoa msaada kwa waathiriwa wa mateso ya nyumbani .

Bi Go na mashirika mengine ya haki za wanawake nchini Korea wanahoji kuwa nchi hiyo ina tatizo la unyanyasaji wa kingono ambalo linahitaji uangalizi wa haraka. "Inaenea katika tamaduni zetu," alisema, akiongeza kuwa wanaume walikuwa na fursa nyingi za kuelezea mapenzi yao bila kuhitaji tamasha kufanya hivyo.

Bae Jeong-weon, ambaye anafundisha masuala ya kujamiiana na utamaduni katika Chuo Kikuu cha Sejong, alisema moja ya masuala ya tamasha hilo ni kwamba lililenga zaidi hadhira ya wanaume.

"Kuna ukatili mwingi dhidi ya wanawake hapa, na hivyo wanawake wanahusika zaidi na masuala ya kuwanyanyasa," alisema. Katika utafiti wa mwaka wa 2022 wa wizara ya jinsia ya serikali, zaidi ya thuluthi moja ya wanawake walisema walipitia unyanyasaji wa kijinsia.

"Nchini Korea Kusini tuna historia ya kuzungumza kuhusu ngono vibaya, katika suala la unyanyasaji na kuwatumia vibaya wanawake, badala ya kukiona kama kitendo chanya, cha kufurahisha," Bi Bae aliongeza.

Huko Gangnam, ambapo tamasha lilipaswa kufanyika, wakazi wa kitongoji hicho wengi wao wakiwa vijana walionekana kugawanyika kulingana na jinsia zao. "Siyo ponografia na hawafanyi chochote kinyume cha sheria, kwa hivyo sidhani kama ingepaswa kuzuiwa," alisema mfanyakazi wa kiume wa IT Moon Jang-won. Lakini Lee Ji-yeong mwenye umri wa miaka 35 alisema anasikitikia mabaraza mbalimbali na "alichukizwa na tamasha hilo kwa kufanya biashara ya ngono".

Lakini wengi walikubali kwamba kwa kupiga marufuku tamasha hilo, mamlaka zilivuka mipaka.

Waandamanaji wanasema sekta ya ngono inahimiza unyanyasaji dhidi ya wanawake.
Waandamanaji wanasema sekta ya ngono inahimiza unyanyasaji dhidi ya wanawake.

"Marufuku hii ilikuwa uamuzi wa wanasiasa wazee, wahafidhina ambao wanataka kuwavutia wapiga kura wazee," alisema Yoo Ju mwenye umri wa miaka 34. "Kizazi hiki bado kinaamini kuwa ngono lazima ifichwe," aliendelea, akiongeza kuwa mitazamo ya vijana kuhusu ngono ilikuwa ikibadilika, na kwamba yeye na marafiki zake walizungumza waziwazi kuhusu suala hilo.

Siasa nchini Korea Kusini bado inaongozwa kwa kiasi kikubwa na maadili ya kihafidhina, ya jadi .Mwaka jana, baraza la jiji la Seoul lilisimamisha Queer Pride kuzuiliwa kwenye uwanja mkuu wa jiji kufuatia upinzani kutoka kwa vikundi vya Kikristo. Serikali bado haijapitisha sheria ya kupinga ubaguzi ambayo italinda jamii ya watu wa kabila na wanawake, ambao wote wanakabiliwa na chuki kubwa.

Mzozo kuhusu tamasha la ngono umesababisha maswala haya mawili ya tofauti za kijinsia na usawa wa kijinsia kuingizwa, na waandaaji wakibishana kuwa viongozi walikuwa wakiwazuia watu kujieleza kwa uhuru, na wanawake wakidai kuwa haki zao zilikiukwa.

Mamlaka italazimika kujua jinsi ya kushughulikia mtanziko huu mgumu. Play Joker iliiambia BBC kuwa inapanga kujaribu tena kuandaa tamasha hilo mnamo Juni, kubwa zaidi, huku Bw Lee akidai kuwa sasa ana wanasiasa kadhaa walio upande wake. Mwishoni mwa wiki, meya wa Seoul alitoa taarifa kwenye chaneli yake ya YouTube akisema jiji hilo "halikuwa na nia ya kuingilian tena katika siku zijazo".

Ripoti ya ziada ya Jake Kwon na Hosu Lee.Imetafsiriwa na Yusuf Jumah