Marekani yampongeza Ruto kwa kubadili msimamo kuhusu Mswada wa Fedha 2024

Taarifa zinasema Blinken alimsifu Bw. Ruto kwa hatua aliyochukuwa kuhakikisha amani inadumishwa nchini.

Muhtasari
  • Wawili hao walifanya mazungumzo baada ya Rais Ruto kukubali shinikizo kutoka kwa Wakenya kutupilia mbali Muswada wa Fedha wa 2024.
Image: screengrab

Rais William Ruto na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken wameripotiwa kuwasiliana kwa njia ya simu.

Wawili hao walifanya mazungumzo baada ya Rais Ruto kukubali shinikizo kutoka kwa Wakenya kutupilia mbali Muswada wa Fedha wa 2024.

Taarifa zinasema Blinken alimsifu Bw. Ruto kwa hatua aliyochukuwa kuhakikisha amani inadumishwa nchini.

“Waziri Blinken alimshukuru Rais Ruto kwa kuchukua hatua za kupunguza mivutano na akaahidi kushiriki mazungumzo na waandamanaji na mashirika ya kiraia,” taarifa kutoka kwa Msemaji wake ilisema.

Blinken alisisitiza umuhimu wa vyombo vya usalama kujizuia ili kuepusha aina yoyote ya vurugu.

Pia alitoa wito wa uchunguzi wa haraka kuhusu ukiukwaji wowote wa haki za binadamu.