Mwanaume ashtakiwa kwa kuvunja simu ya mrembo aliyemkataa

Muhtasari

• Mwansume mmoja alifikishwa katika mahakama ya Kibera na kushtakiwa kwa kuvunja simu ya mwanamke aliyemkataa kimapenzi.

Mahakama
Mahakama
Image: MAKTABA

Mwanaume mmoja alipandishwa kizimbani katika mahakama ya Kibera jijini Nairobi baada ya kupasua simu ya mwanamke ambaye alimkataa kimapenzi.

Mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina Justin Okari alijjipata pabaya baada ya kufika katika biashara ya mwanamke huyo anayedaiwa kuwa mpenzi wake wa zamani na ambaye alikatisha mahusiano yao, na kupasua simu ya mwanamke huyo huku akimnyea matusi.

Inadaiwa Okari alifika na kumtaka mwanamke huyo kutoka na yeye ili kuelekea katika nyumba ya mshatakiwa iliyopo katika barabara ya Ngong ambapo mwanamke alikataa na hapo ndipo Okari alipandisha mori na kuzusha timbwiri kama lote, mpaka kumpokonya simu ghafla na kuigongesha chini kwa sakafu ya saruji.

Okari alifikishwa katika mahakama ya Kibera na kusomewa mashtaka ya kuharibu mali ya mtu kwa kukusudia, mashtaka ambayo aliyakanusha na kuachiwa kwa dhamana ya pesa taslimu elfu 50 au bondi mbadala ya laki moja.

Kesi hiyo itaendelea tena mnamo April 6.