Picha na video za uchi za seneta Linturi zafutwa, mahakama yaambiwa

Muhtasari

• Mpelelezi mkuu katika kesi hiyo Keith Roberts amesema kuwa wanachunguza kuharibiwa kwa picha na video za Linturi.

• Katika hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani, afisa wa polisi Keith Robert anasema wanaamini kuwa mbunge huyo alichangia pakubwa katika kufuta picha hizo za uchi.

Seneta wa Meru Mithika Linturi ameachiliwa kwa bondi ya Sh5 milioni na mdhamini wa kiasi sawa na hicho na dhamana mbadala ya Sh2milioni pesa taslimu.
Seneta wa Meru Mithika Linturi ameachiliwa kwa bondi ya Sh5 milioni na mdhamini wa kiasi sawa na hicho na dhamana mbadala ya Sh2milioni pesa taslimu.
Image: Jeptum Chesiyna

Mpelelezi mkuu katika kesi ya jaribio la ubakaji dhidi ya Seneta wa Meru Muthika Linturi amedai kuwa afisi yake inachunguza madai ya kuharibu picha na video za uchi za kisa hicho.

Katika kesi hiyo Linturi ameshtakiwa kwa jaribio la ubakaji ambapo inadaiwa aliingia katika chumba cha hoteli cha mwathiriwa na kujaribu kumbaka mwanamke huyo wakati mumewe akiwa nje.

Katika hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani, afisa wa polisi Keith Robert anasema wanaamini kuwa mbunge huyo alichangia pakubwa katika kufuta picha hizo za uchi.

Robert's ameiambia mahakama kuwa uchambuzi wa kisayansi unafanyiwa simu za rununu ili kupata data iliyopotea.

Hata hivyo, ameambatanisha video mbili ambazo zilichukuliwa katika eneo la tukio.

Aliendelea kusema kuwa uchunguzi kuhusu malalamishi ya mwathiriwa ulifanyika kwa bila kuegemea upande wowote na kwa madhubuti upatikanaji ya haki.

Ameiomba mahakama kutupilia mbali ombi la Linturi la kutaka kusitisha kesi ya jaribio la ubakaji kwa madai kuwa polisi wameshindwa kutoa hati walizo nazo.

Anasema kusitisha kesi hiyo hakutampa mwathiriwa Haki anayostahili.

Linturi pia alitaka upande wa mashtaka kutoa stakabadhi za matukio katika kituo cha polisi cha Nanyuki, picha zake za uchi na video ambazo mwathiriwa na mumewe walichukua.