Mwanamume akamatwa kwa kutaka kumtoa bintiye kafara

Muhtasari
  • "Wakati huo huo, mshukiwa yuko chini ya ulinzi wa polisi akisaidia katika uchunguzi," waliongeza
Pingu
Image: Radio Jambo

Polisi nchini Nigeria mnamo Ijumaa walimkamata mfanyabiashara mmoja kwa madai ya kujaribu kumuua bintiye kwa tambiko.

Evans Oppong, 42, mkazi wa Fise karibu na Amasaman, alinaswa baada ya polisi kupata habari kwamba alimpeleka bintiye mwenye umri wa miaka 11 kwa kasisi wa kimila huko Oyibi Kom huko Accra, kwa madhumuni ya ibada siku ya Alhamisi.

"Tunamshukuru raia huyo mzalendo aliyetoa taarifa iliyopelekea kukamatwa kwa huduma yake ya kujitolea ambayo iliokoa maisha ya mtoto aliyehusika," polisi walisema. Pia walisema mwathiriwa alikuwa salama na wanafanya kazi ya kumuunganisha na familia yake.

"Wakati huo huo, mshukiwa yuko chini ya ulinzi wa polisi akisaidia katika uchunguzi," waliongeza.

Nana Adu-Boafo Jnr, mganga wa mitishamba, alisema alishtuka Oppong alipomletea bintiye akidai alitaka atolewe dhabihu kwa pesa.

Ilimsukuma kuwaarifu polisi.

"Aliniahidi GHc 10,000 na vitu vingine vya kushangaza baada ya ibada," Boafo Jnr alisema katika chapisho la Facebook.

Aliwaambia polisi, Oppong alimwambia kwamba alisafiri hadi Nigeria kwa malisho ya kijani kibichi, katika juhudi za kupata pesa zaidi.

Oppong anasemekana kumtoa bintiye shuleni akidai alitaka kumpeleka nje kwa ununuzi wa nguo.

Boafo alisema kuwa mwanamume huyo pia alikuwa amepanga kumtoa dhabihu mtoto wake mwingine, kwani yeye ni baba wa watoto 12.

"Huyu ni mtu mbaya mwenye nia nyingi ovu. Hajisikii chochote kwa msichana wake mwenyewe," Boafo alisema.

Kesi hiyo itasikizwa Juni 20, 2022.