Mashahidi 2 kutoa ushahidi katika kesi ya ufisadi ya Waititu kabla ya kufungwa

Waititu, mkewe Susan Wangari na wengine 11 wanakabiliwa na kesi kuhusu utoaji wa zabuni ya barabara

Muhtasari
  • Vyombo vya uchunguzi vinasema zabuni hiyo ilitolewa kwa njia isiyo ya kawaida na hivyo ndivyo suala hilo lilifika mahakamani.
Aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu
Aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu
Image: MAKTABA

Upande wa mashtaka umesalia na mashahidi wawili zaidi kabla ya kuhitimisha kesi ya ufisadi ya Sh588 milioni inayomkabili aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu na wengine.

Wawili hao ni mkaguzi wa hati na afisa wa uchunguzi.

Msaidizi huyo alipaswa kufika kortini Jumatano lakini upande wa mashtaka Jumanne uliiomba mahakama kuruhusu ombi lao la kuahirishwa kwa kuwa shahidi hangepatikana.

Mahakama ilisikia kwamba shahidi huyo atashughulikia suala tofauti huko Homa Bay. Kufikia sasa, mashahidi 27 wametoa ushahidi katika kesi hiyo.

Hakimu wa kesi Thomas Nzyuki aliruhusu ombi lao akisema upande wa mashtaka unapaswa kuhakikisha shahidi atakuwa kortini Juni 5, kesi itakaporejelewa.

Hakimu Mashauri alisema hata kama hatapatikana, basi upande wa mashtaka unatakiwa kumpatia ofisa mpelelezi ili atoe ushahidi wake katika kesi hiyo.

Waititu, mkewe Susan Wangari na wengine 11 wanakabiliwa na kesi kuhusu utoaji wa zabuni ya barabara za Sh588 milioni katika kaunti ya Kiambu kinyume cha sheria.

Zabuni inayohusika ilitolewa Februari 12, 2018, na kupewa Testimony Enterprise inayomilikiwa na wakurugenzi wake—Charles Chege na Beth Wangeci-baada ya kunukuu Sh588 milioni.

Ilikuwa kwa ajili ya uboreshaji wa barabara mbalimbali za changarawe katika kaunti za Thika, Limuru, Gatundu Kaskazini, Juja, na Ruiru katika mwaka wa kifedha wa 2017-2018.

Vyombo vya uchunguzi vinasema zabuni hiyo ilitolewa kwa njia isiyo ya kawaida na hivyo ndivyo suala hilo lilifika mahakamani.