Mackenzie afikishwa mahakamani baada ya kukaa rumande kwa siku 30

Hakimu Yusuf Shikanda aliruhusu polisi kuwashikilia Mackenzie, mkewe Rhoda Maweu, na washtakiwa wengine 16 kuhusiana na vifo vya zaidi ya watu 240.

Muhtasari

•Kiongozi wa kanisa tata la Malindi Paul Mackenzie na washukiwa wenzake wengine 17 wamefikishwa mahakamani.

Mchungaji Paul Mackenzie

Baada ya kukaa chini ya ulinzi wa polisi kwa zaidi ya mwezi mmoja, kiongozi wa dhehebu tata la Malindi Paul Mackenzie na washukiwa wenzake wengine 17 wamefikishwa mahakamani.

Mwezi uliopita, Hakimu Mkuu Mwandamizi Yusuf Shikanda aliruhusu polisi kuwashikilia Mackenzie, mkewe Rhoda Maweu, na washtakiwa wengine 16 kuhusiana na vifo vya zaidi ya watu 240 waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola.

DPP na DCI walikuwa wameomba angalau siku 90 kuwachunguza washukiwa lakini wakapewa siku 30 ambazo zilikatika siku ya Ijumaa.