Baba aliyefungwa maisha kwa kosa la kumnajisi bintiye aachiliwa huru

Alihukumiwa maisha mnamo Machi 9, 2022, na Mahakama ya Kilungu baada ya bintiye kumshtaki kwa kumnajisi.

Muhtasari

• Alidai kuwa hakimu alikosea kumtia hatiani licha ya kutokuwepo kwa ushahidi kuthibitisha ikiwa alifanya kosa hilo.

Mahakama
Mahakama
Image: MAHAKAMA

Mwanamume aliyekuwa amefungwa kwa madai ya kushiriki mapenzi na bintiye sasa ako huru baada ya kuwa jela kwa karibu mwaka mmoja.

*Stephen (si jina lake halisi) alihukumiwa kifungo cha maisha mnamo Machi 9, 2022, na Mahakama ya Kilungu baada ya bintiye kumshtaki kwa kumnajisi.

Msichana mwenye umri wa miaka 16 *Mary (si jina lake halisi) alidai kuwa babake alimnajisi kwa tarehe tofauti kati ya Mei na Agosti 2018 eneo la Mukaa, Makueni.

Baada ya kusikilizwa kwa kesi, mwanamume huyo alipatwa na hatia na kuhukumiwa, licha ya kusisitiza kuwa hakufanya kosa hilo.

Akiwa amedhamiria kupinga uamuzi wa mahakama hiyo, Stephen aliwasilisha ombi katika Mahakama Kuu ya Makueni na kukata rufaa.

Alidai kuwa hakimu alikosea kumtia hatiani licha ya kutokuwepo kwa ushahidi kuthibitisha ikiwa alifanya kosa hilo.

Alisema kuwa bila ushahidi huo, upande wa mashtaka hauwezi kuthibitisha kosa la kujamiiana na bintiye.

Pia alimlaumu hakimu kwa kuhamisha mzigo wa uthibitisho kwake na kusababisha uamuzi usiyo sahihi.

Stephen alimwambia Jaji George Dulu kwamba mahakama ya mwanzo imeshindwa kuona kwamba ushahidi wa upande wa mashtaka haukubaliki, haustahili, unakinzana na umejaa uongo.

Alipopitia masuala yaliyoletwa mbele ya mahakama na kesi hiyo, hakimu aligundua kwamba ushahidi wa Mary kuhusu kujamiana na babake haukuwa wa kuaminika.

Alihoji kwamba ripoti zote za awali na kesi ya awali ya uhalifu dhidi ya Stephen ilikuwa kuhusu yeye kujaribu kusaidia kuavya mimba.

"Sijaambiwa kama kesi ya awali ilimalizika kwa kuachiliwa, kutiwa hatiani au kuiondoa. Kwa namna yoyote ile, ni wazi kwangu kwamba kesi hii ya baadaye dhidi ya aliyewasilisha rufani ilikuwa ni mawazo ya baadaye na msingi wa ushahidi wenye mashaka, na mahakama ya mwanzo ilipaswa hivyo basi kumwamini mrufani kwa kiasi fulani,” Jaji aliongeza.

Zaidi ya hayo, hakimu alisema mahakama hiyo ilipaswa kumshtaki babake msichana huyo wakati wa kushtakiwa kwa kosa la kusaidia kutoa mimba. Hii ni kwa sababu ukweli ulikuwa katika mfululizo sawa na kesi ya awali.

"Kwa kifupi, itakuwa rahisi sana kwa mtu kushtakiwa mara mbili au zaidi kwa makosa sawa au mfululizo, na kusababisha hatari mara mbili, kinyume na kanuni za hukumu ya haki," mahakama ilisema.

Kwa kumalizia na katika hukumu iliyotolewa Januari 11, Jaji Dulu aliruhusu rufaa hiyo, na kufutilia mbali hukumu hiyo.

“Ninaamuru kwamba mrufani aachiliwe huru mara moja,” hakimu aliamuru.