Mzalendo Kibunja na wengine watatu wakamatwa kwa madai ya kufuja pesa za makavazi ya kitaifa

Kibunja na maafisa wengine wawili wa makavazi ya kitaifa walikamatwa siku ya Jumatatu na makachero wa EACC.

Muhtasari

• Wanne hao walizuiliwa katika kituo cha polisi cha EACC Integrity Center wakisubiri kufikishwa mahakamani Jumanne.

Makao yatume ya maadlili na kupambana na ufisadi
EACC Makao yatume ya maadlili na kupambana na ufisadi
Image: MAKTABA

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Makavazi ya Kitaifa ya Kenya Mzalendo Kibunja anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo Jumanne kujibu mashtaka ya ufujaji wa pesa za umma.

Kibunja na maafisa wengine watatu wa makavazi ya kitaifa walikamatwa siku ya Jumatatu na makachero wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kwa madai ya ufujaji wa shilingi 490 milioni.

Kibunja alikamatwa pamoja na maafisa wengine watatu wa Makavazi ya Kitaifa ya Kenya, miongoni mwao Oliver Okinyi, afisa wa ICT na Oscar Mwaura.

Mwaura anasemekana kuongoza zoezi la kuajiri wafanyakazi hewa ambao walilipwa pesa ambazo baadaye zilielekezwa kwenye akaunti za watu binafsi.

Ubadhirifu huo unasemekana ulifanyika kwa kipindi cha miaka mitano.

Wanne hao walizuiliwa katika kituo cha polisi cha EACC Integrity Center wakisubiri kufikishwa mahakamani Jumanne.

EACC ilisema kwamba iko tayari kuanzisha mchakato wa kurejesha rasilimali zilizoibiwa.