Shule kulipa fidia ya Ksh 650k kwa kumfukuza mwanafunzi wa miaka 12 mwenye virusi vya HIV

Uongozi wa shule hiyo ya msingi ulimfukuza shuleni mwanafunzi huyo wa kiume baada ya kubaini kwamba ni mwathirika wa ugonjwa huo, jambo ambalo wazazi wake walidai lilimuathiri pakubwa kisaikolojia mwanao.

Muhtasari

• Kwa mujibu wa taarifa, Mvulana huyo alikuwa akitumia dawa za kurefusha maisha (ARVs) kwa siri akisaidiwa na kaka yake mkubwa shuleni.

• Mara tu shule ilipojua kuhusu hali yake, walimfukuza na kudaiwa kumpa mamake KSh10,000 ili aondoke shuleni.

Image: THE STAR

Mahakama mjini Garissa imeitaka shule moja kulipa fidia ya Zaidi ya laki 6 kwa familia ya mwanafunzi wa miaka 12 ambaye anaishi na virusi vya HIV.

Inaarifiwa kwamba uongozi wa shule hiyo ya msingi ulimfukuza shuleni mwanafunzi huyo wa kiume baada ya kubaini kwamba ni mwathirika wa ugonjwa huo, jambo ambalo wazazi wake walidai lilimuathiri pakubwa kisaikolojia mwanao.

Mahakama ya kutatua kesi za unyanyapaa dhidi ya waathirika wa HIV ilipata uamuzi wa shule wa kumfukuza mwanafunzi wa Darasa la Pili kwa sababu ya hali yake ya VVU kuwa usio wa haki.

Kwa mujibu wa taarifa, Mvulana huyo alikuwa akitumia dawa za kurefusha maisha (ARVs) kwa siri akisaidiwa na kaka yake mkubwa shuleni. Mara tu shule ilipojua kuhusu hali yake, walimfukuza na kudaiwa kumpa mamake KSh10,000 ili aondoke shuleni.

Mama huyo alisema kuwa shule hiyo ilitoa KSh600 pekee, na mwanawe akaacha kwenda shule kutokana na ubaguzi uliomsababishia mfadhaiko.

Mahakama hiyo ilihitimisha kuwa tabia ya shule hiyo haikuwa ya haki na kinyume cha sheria, sawa na ubaguzi dhidi ya mtoto, ambayo ni kinyume na Kifungu cha 32 cha Sheria.

Alituzwa (mahakama) KSh400,000 kwa ubaguzi na ziada ya KSh250,000 kwa mateso yaliyosababishwa na shule.