Tazama video yake Omosh akikiri karibu ajiue mwaka jana, na kuwa hana pesa

Muhtasari
  • Omosh afichua kwamba kuna wakai karibu ajiue mwaka jana alipoona maisha yamekuwa magumu

Wasanii,waigizaji na watu mabalimbali mwaka jana walipata hasara kubwa na hata wengine kupoteza kazi baada ya janga la corona kuripotiwa nchini.

Miongoni mwa waigizaji walioathirika ni Joseph Kinuthia almaarufu Omosh, ambaye akiwa kwenye mahojiano na radiojambo alieleza jinsi aling'ang'ana na maisha yake na familia yake huku akiwa na bibi wawili.

Muigizaji huyo alifichua kwamba kuna wakati alikuwa karibu ajiue alipoona maisha yamekuwa magumu.

 
Joseph Kinuthia
Image: Ivy Muthoni

"Karibu nijiue mwaka jana, lakini marafiki zangu walikuja na kunipa ushauri, mimi naishi maisha haya kwa ajili ya marafiki zangu ambao wamekuwa wakinisaidia

kwa sasa sina kazi yeyote , nimesomea kazi ya uhasibu, wake zangu wote wawili wanafanya kazi ya hapa na pale

Kuna wakati ulifika mpaka mwenye nyumba alinitishia kunifukuza kwa ajili sikuwa nimelipa kodi ya nyumba na sikuwa na pesa." Aliongea Omosh.

Omosha alisema kwamba alipokuwa ameingia kulewa hakuwa na uwezo wa kuwashika mono wanawe ilhali wake wake hawajawahi muacha licha ya hayo yote.

Hii hapa video hiyo;

Radio Jambo Kenya | Ongea Usikike | Ni kituo nambari moja Kenya kwa matangazo ya kiswahili. Vipindi vyake vina jumuisha Spoti,Mijadala moto moto na muziki wa Kiafrika #RadioJamboKenya Subscribe to RadioJambo Youtube - https://bit.ly/39wwc6u Mitandao ya Kijamii Instagram - https://rb.gy/e154d1 Facebook - https://rb.gy/09d1b9 Twitter - https://rb.gy/e23220