Mabadiliko ya Katiba hayatafanya kazi ikiwa viongozi hawatakubali kushindwa katika uchaguzi - Ruto

Muhtasari
  • Naibu rais William Ruto asema haya kuhusu kubadilisha katiba
Mtangazaji Gidi na naibu rais William Ruto
Image: Douglas Okiddy

Kenya inapoteza muda na kubadilisha Katiba ikiwa viongozi wake hawatakubali wanaposhindwa katika uchaguzi, haya ni matamshi yake naibu rais alipokuwa kwenye mahojiano na Radiojambo.

Akizungumza Jumanne, Ruto alisema kuwa shida iko kwa watu ambao hawaamini demokrasia na wale ambao hawakubali kamwe wanaposhindwa.

“Shida kubwa iko kwenye uchaguzi. Hata sasa tunapoteza wakati na kubadilisha Katiba .. tunaweza kuibadilisha mara 100 lakini ikiwa anayeshindwa hatakubali bado ataleta maswala na hata kujiapisha, ”alisema.

Pia kigogo huyo alisema kwamba enapo atashindwa kwenye uchaguzi mwaka ujao atakubali, na kama atatangazwa kuwa ameshinda atafurahi sana.

"Mimi kama William Ruto, nitakubali uamuzi wa wakenya. IEBC ikitangaza kwamba nimeshinda, nitafurahi, iwapo itatangazwa kwamba nimeshindwa na mpinzani wangu, nitakubali maanake mimi nina imani na demokrasia...

Image: Douglas Okiddy

Hawa wengine hawawezi maanake hawajawahi kusema kwamba watakubali wakishindwa..."

Ruto alisema kwamba baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2017 kulikuwa na mpango wa kumhangaisha kisisasa.

"Mimi nimeamua, kwa sababu ya heshima kwa nchi, sitaki mvutano kati yangu na rais... Kuna ufisadi mkubwa katika vita vya kupigana na ufisadi kuliko vita dhidi ya ufisadi..."

Watu wakishashindwa na mpango, kulikuwa na mpango baada ya uchaguzi nihangaishwe nisipate uongozi wowote, wanaanza visingizio.

Kama kuna mtu ako na heshima na rais ni mimi, hawa wote wanaoongea eti nimemkosea heshima ni watu wa siasa ya bure."