Mapenzi kizungumkuti

Ex-wangu ashaolewa na bado anataka turudiane kisiri

Utata wa mahusiano ya kale

Muhtasari
  • Ephraim ambaye baada ya kuachana  na Naomi miaka  takriban mitatu iliyopita ,anashangaa kwamba mwanadada huyo yungali anamsumbua katika mitandao ya kijamii na hata kumpigia simu akitaka warudiane
  • Tatizo ni kwamba tayari  Naomi ni mke wa mtu!
  • Ephraim anasema yungali anampenda Naomi lakini kufahamu kwamba ana mume ,ni jabo linalompa woga  wa kufanya lolote linaloweza kumletea matatizo

 

sad man
sad man

Kunao watu ambao wana ujasiri ama hawana haya kabisa . Hebu fikiri kuhusu kumuacha mtu bila sababu  tosha kisha baadaye ukiwa ushaolewa uanze tena kumsumbua kwamba unataka mrudiane. Ndio yanayomsibu Ephraim ambaye baada ya kuachana  na Naomi miaka  takriban mitatu iliyopita ,anashangaa kwamba mwanadada huyo yungali anamsumbua katika mitandao ya kijamii na hata kumpigia simu akitaka warudiane . Tatizo ni kwamba tayari  Naomi ni mke wa mtu!

Emphraim anasema kinachomshangaza ni  hatua ya Naomi kumuacha bila sababu baada ya kuwa katika uhusiano kwa Zaidi ya miaka miwili pindi walipomaliza masomo ya chuo kikuu . Anasema walitengana bila hata sababu kwa  ajili anachokumbuka ni kwamba Naomi alitaka muda wa  kupumzika kutoka uhusiano huo akidai kamba hakuwa na furaha ndani ya uhusiano wake . Sasa Ephraim alijua labda baada ya muda Fulani akipata pumzi zake wangeweza kushughulikia mambo ya kuboresha uhusiano wao kisha waendelee na mapenzi yao .

  Muda sio mrefu alisikia kwamba Naomi alikuwa kashahamia Eldoret na hata akapata mume . Muda wote huo Ephraim alikwaza lakini hata machungu ya moyo wake yalikuwa yashapona . Bila hata kutarajia ,siku moja  anaanza kutumiwa jumbe na mwanamke katika facebook . Alipoangaliwa makini akagundua ni Naomi –mpenzi wake wa zamani ambaye ndiye aliyekuwa akiwasiliana naye . baada ya  gumzo la hapa na pale kujuliana hali ,Naomi alianza kurejesha mazungumzo kuhusu jinsi anavyompenda na angetaka warudiane . Ephraim anasema mwanzoni alikuwa akipuuza  maneno yake akifikiri anafanya utani lakini muda ulivyowenda ,naomi alidhihirisha wazi kwamba hakuwa  anafanya mzaha na kwa kweli alitaka tena kurudiana naye . Tatizo ni kwamba hata Ephraim angekubali ,huyu sasa ni mke wa mtu na ingekuwa sio sawa kurudia uhusiano kama huo kwani ungekuwa na athari nyingi  sio kwake tu bali kwa wote .

 Kinachomtisha sana  Ephraim ni kujua mbona Naomi anataka kutoroka mume wake wa miaka mitatu ili kurudiana naye ilhali alimuacha bila sababu licha ya uhusiano ya mapenzi yao yaliodumu miaka miwili hapo awali .

 Ephraim anasema yungali anampenda Naomi lakini kufahamu kwamba ana mume ,ni jabo linalompa woga  wa kufanya lolote linaloweza kumletea matatizo .