Tahadhari

Unajua mwanao hufanyiwa nini na msichana wa kazi?

Baadaye alimpeleka mtoto wake hospitalini na alipoangaliwa na daktari ,ilibainika kwamba mtoto huyo alikuwa amedhulumiwa kimapenzi

Muhtasari
  • Anasema mtoto wake alimuonyesha jinsi ‘Auntie’ humwambia  amlambe  sehemu zake za siri na wakati mwingine ‘kuvuta dudu yake’ na kujitilia katika sehemu zake za siri
  • Grace  Msambo amesimulia jinsi mtoto wake mwenye umri wa miaka saba alivyomsimulia mambo ya kushtusha ambayo yeye hufanyiwa na msichana wa kazi wakati anapokuwa amekwenda kazini .

Mwanamke mmoja ametumnia mtanadao wa facebook kuwaonya akina mama  wenzake kuwa wangalifu wanapowaacha wanao hasa wa kiume na wafanyikazi wa nyumbani wa kike .

Grace  Msambo amesimulia jinsi mtoto wake mwenye umri wa miaka saba alivyomsimulia mambo ya kushtusha ambayo yeye hufanyiwa na msichana wa kazi wakati anapokuwa amekwenda kazini .

Anasema mtoto wake alimuonyesha jinsi ‘Auntie’ humwambia  amlambe  sehemu zake za siri na wakati mwingine ‘kuvuta dudu yake’ na kujitilia katika sehemu zake za siri . Anasema mwanzoni alishangaa mtoto wake alijuaje vitu vikubwa kama hivyo lakini baada ya kumzikiliza kwa makini na kumhoji mfanyikazi wake wa nyumbani ,aligundua kwamba mtoto wake wa kiume alikuwa akidhulumiwa kimapenzi  na msichana wao wa kazi .

Grace anasema ufichuzi wa mtoto wake kuhusu kilichokuwa kikifanyika ulimuacha na butwaa asijue la kufanya lakini   baada ya kumuuliza mfanyikazi wake maswali ,hakuweza kumpa majibu ya kuridhisha na pale alijua la kufanya kwani mara moja bila kusita alimfungisha virago mfanyikazi wake huyo .

Baadaye  alimpeleka mtoto wake hospitalini na alipoangaliwa na daktari ,ilibainika kwamba mtoto huyo alikuwa amedhulumiwa kimapenzi kwani maelezo aliotoa yalionyesha wazi kwamba mfanyikazi yule wa nyumbani alikuwa  akimtumia vibaya mtoto kwa kufanya naye tendo la utu uzima pasi na mtoto kujua kwamba jambo hilo halikumfaa na umri wake .

Visa vya watoto wavulna kudhulumiwa kimapenzi na wasichana wa kazi majumani sio vigeni kwani pametpokea ripoti nyingi za jinsi watoto wengi hudhulumiwa kimapenzi bila wazazi wao kufahamu .Kuna Tukio hata ambalo mfanyikazi wa nyumbani alimuambukiza mtoto wa miaka 12 ugonjwa wa zinaa baada ya kushiriki naye tendo la utu uzima na baadaye mtoto alipolemewa kwa kupata uchungu akienda haja ndogo ndipo alipofichua kilichokuwa kikifanyikazi .

Kando na dhulma hizo na kingono ,wazazi pia wanafaa kuwa wangalifu kuhusu mateso na kupigwa kwa wanao wakati wanapowaacha chini ya utunzi na malezi ya wafanyikazi wa nyumbani .