- Kenya ilianzisha matumizi ya DTG mwaka jana ili kuziba nafasi ya dawa nyingine za ukimwi kama dawa msingi ya matibabu .
- Takwimu kutoka tafiti mbili zilizofanywa Kenya ,Afrika Kusini na Cameroun zimeonyesha ongezko kubwa la uzani wa watumiaji wa dawa hiyo .
Dawa mpya ya HIV kwa jina Dolutegravir inakabiliwa na changamoto mpya baada ya utafiti kuonyesha kwamba inasababisha wanawake kunenepa .
Pia haisaidii kupunguza virusi kwa watu ambao tayari miili yao ilikataa kukubali dawa nyingine za HIV .
Hata hivyo Dolutegravir, ambayo pia inajulikana kama DTG inasalia kuwa dawa yenye uwezo zaidi kukabiliana na virusi vya HIV na mseto wake unapendekezwa na WHO kwa watu walio na HIV .
Kenya ilianzisha matumizi ya DTG mwaka jana ili kuziba nafasi ya dawa nyingine za ukimwi kama dawa msingi ya matibabu .
Takwimu kutoka tafiti mbili zilizofanywa Kenya ,Afrika Kusini na Cameroun zimeonyesha ongezeko kubwa la uzani kwa watumiaji wa dawa hiyo .
Utafiti wa kwanza uliofanywa na African Cohort Study, uliwahusisha watumiaji 2000 kati ya januari mwaka wa 2013 na Novemba mwaka wa 2019 katika kliniki 12 zinazosaidiwa na Pepfar- katika nchi za Kenya, Nigeria, Tanzania na Uganda.
Watu waliotumia mchanganyiko wa Dolutegravir/TDF/Lamivudine walikuwa na uwezo wa asilimia 85 kuongeza uzani kuwaliko waliokuwa wakitumia dawa zisizo na mchanganyiko wa dolutegravir
Vile vile wale waliokuwa chini ya matumizi yay a DTG walikuwa na uwezekano wa asilimia 27 kupata hyperglycemia-mkurupuko wa sukari kupindukia katika damu unaohusishwa na maradhi ya kisukari .
Katika utafiti wa Afrika kusini na Cameroun iligunduliwa kwamba wanaume waliokuwa wakitumia mseto wa DTG walipata ongezeko la uzani wa kilo tano .
Wanawake waliongeza kilo nne hadi nane
DTG inasalia kuwa dawa yenye ufanisi zaidi sokoni ya ARV
Imesajili uwezo mkubwa wa matokeo ,ni rahisi kutumia na ina athari chache za kando ikilinganishwa na dawa mbadala ,kulingana na shirika la Afya Duniani WHO .
Dawa hiyo inatengezwa na ViiV Healthcare, kampuni yenye makao yake nchini Uingereza ambayo inashughulika na dawa za kutibu HIV .
Asilimia 76 ya kampuni hiyo inamilikiwa na GlaxoSmithKline, asilimia 13.5 na Pfizer na asilimia 10 na Shionogi ya Japan.