Vipimo vya DNA

Kabla ya kujiita ‘baba watoto’ hakikisha una ithibati kwamba watoto ni wako

Mume wake alipoanza kusikia uvumi huo kwamba watoto wale hawakuwa wake ,aliamua kufaya vipimo vya DNA .

Muhtasari
  • Wakati mahakama ilipofanya uamuzi kuhusu hifadhi ya watoto ufichuzi huo haukutolewa na kila mtu alijua kwamba  baba yao ndiye aliyekuwa baba mzazi .
  •  Ilikuwa kesi kali na  iliyowavutia watu wengi ambao waliifuatilia kwa makini wakitaka kujua uamuzi wa mahakama

 

 

 Usije ukapatwa na mshangao siku moja kwa sababu maisha yanaweza kukupa somo  .Unaweza kupigania kitu kumbe hujui kwamba hakikufaa vita  vyote na muda wote huo . Ndio masiabu ya mwanamme mmoja ambaye mke wake wa zamani amefichua jinsi alivyokwenda mahakamani akitaka kusalia na watoto wao wakati walipotalakiana .

 Ilikuwa kesi kali na  iliyowavutia watu wengi ambao waliifuatilia kwa makini wakitaka kujua uamuzi wa mahakama . Alice* Alikuwa ameamua kumtaliki mumewe baada ya ndoa yao iliyodumu miaka 14 na tofauti ikaibuka kato yao kuhusu atakayepewa idhini ya mahkama kwenda na watoto wao wawili ambao wakati huo walikuwa katika shule ya msingi . kwa sababu mumewe alikuwa akifanya kazi katika makao makuu ya mkoa siku hizo ,alikuwa na pesa na pia ushawishi hivyo basi kesi ilipofanywa alipewa ruhusa ya kwenda na watoto wake .

 

 Bila kujua hata hivyo ,wale watoto hawakuwa wake wa kuzaa kwa sababu mapema katika ndoa yao Alice aligundua kwamba mume wake alikuwa  hana uwezo wa kuzalisha na akaamua kutumia njia za kijanja kushika mimba ya mwanamme wa pembeni  huku akisingizia kwamba mume wake ndiye aliyekuwa baba ya watoto wake . wakati mahakama ilipofanya uamuzi kuhusu hifadhi ya watoto ufichuzi huo haukutolewa na kila mtu alijua kwamba  baba yao ndiye aliyekuwa baba mzazi .

Miaka kadhaa badaye wakati watoto walipomaliza masomo ya shule ya upili , Alice alianza kuwatumia jamaa zake kufikisha ujumbe kwa mumewe na njia za kejeli akimcheka kwamba basi alipigania watoto ambao sio wake . Alice alisema mume wake alistahili adhabu hiyo kwani alimpokonya wanawe huku akipata agizo la mahakama kumzuia mama yao kuwaona watoto katika kipindi takriban cha miaka 4 hai walipotimu umri wa miaka 18 kujiamulia iwapo walitaka kumuona mama yao .

 Mume wake alipoanza kusikia uvumi huo kwamba watoto wale hawakuwa wake ,aliamua kufaya vipimo vya DNA .  matokeo yalipkuja kwa kweli ilikuwa ni huruma kwa upande wake kwani thibitisho kwamba wale watoto hawakuwa wake lilimaliza nguvu na kuanzia pale afya yake ikadhoofika kabisa . Jamaa za mume wa Alice  wa zamani walimlani kwa masaibu yaliomkumba  kijana wao na hadi leo uhasama mkubwa bado upo huku watoto wake pia wajipata ndani ya zogo hilo la kutojua baba yao halisi huku wakigundua kwamba waliyemjua kama baba alikuwa tu mlezi wao .

 

Simu za mkononi sasa zimekuwa kama sumu kwa mahusiano na ndoa .Ukiteleza ujipate umepitishamacho katika jumbe za simu za mwenzako basi utakuwa na bahati kuendelea katika uhusiano huo .

Kuna hali zinazokulazimisha kuwa mbali na mpenzi wako au mwenzako wa ndoa .Changamoto hiyo ya umbali hutishia uhusiano.Ni vipi unavyoweza kuziepuka changamoto hizo? #PodiyaYusufJuma#YusufJuma#Longdistancelove Shirikiana,Wasiliana,Ungana au tangamana na Yusuf Juma Facebook:Yusuf Juma/Yusuf Juma-Kenya Instagram:@yusufjumaofficial Twitter:@YusufJumaKenya Email:yusufjuma86@gmail.com