Njia ya mkato

Hawataki kusoma :Soma kuhusu jinsi baadhi ya wasichana wanavyopata gredi za juu vyuoni

Njia rahisi ya kupewa alama wakati wa mtihani ilikuwa ni kuanza kushiriki ngono na mmoja wa wahadhiri wake

Muhtasari
  • Anasema kwamba alilazimika kulala na takriban wahadhiri watatu tofauti walioahidi kumpa alama za juu katika mtihani kwa sababu walifahamu kwamba hakuwa na muda wa kusoma .
  •  Akijitetea Brenda anasema wakati alipokuwa chuoni ,maisha kwake yalikuwa magumu na wakati mwingi alikuwa akifnya kazi za hapa na pale ili kujikumu kimaisha n ahata kulipa sehemu ya karo yake

 

 

Brenda Nzomo  hana soni kuhusu mkataba aliofanya na mhadhiri wake wakati alipokuwa chuo kikuu kwani anasema shughuli zake zilikuwa nyingi  ana hivyo basi hangeweza kusomea  mtihani wake na kupita . Njia rahisi ya kupewa alama  wakati wa mtihani ilikuwa ni kuanza kushiriki ngono na mmoja wa wahadhiri wake ambaye alikuwa akimpa alama za bure bila kujali iwapo amejibu maswali kama ilivyohitajika .

Brenda anasema hilo halikuwa jambo la kushtua kwa saabu aligundua mtindo huo ulikuw ukitumika sana  na wanafunzi wenzake wa kike   na anasema hakuona haja ya kujisumbua kusomea mtihani ilhali wenzake waliokuwa wakilala na wahadhiri ili kupewa alama walikuwa wakimshinda wakati  matokeo yanapotolewa .

Anasema alikuwa akiwahurumia wanafunzi wenzake wa kiume ambao hawakuwa na cha kuwapa wahadhiri wengi walioonekana kuvutiwa na wasichana wa chuoni na kila mmoja alifahamu kwamba wasichana wengi walikuwa wakiibadilisha miili yao na alama katika mtihani . Brenda hakujua kwamba kutakuwa na athari yake na wakati  wa mwaka wake wa tatu aligundua kwamba mhadhiri ambaye alikuwa  akifanya naye  mapenzi ili  ampe alama katika mtihani alikuwa pia akishiriki mapezi na wanafunzi kadhaa wa kike katika darasa lake na madarasa mengine chuoni humo .

Hilo lilianza kumpa hofu ya  uwezekano wa kuambukizwa maradhi ya zinaa lakini cha kumtisha hata Zaidi ni wakati aliposikia wkamba kuna mwanafunzi wa kike aliyelazimika kuavya mimba baada ya kupewa uja uzito na mhadhiri wao .

 Akijitetea Brenda anasema wakati alipokuwa chuoni ,maisha kwake yalikuwa magumu na wakati mwingi alikuwa akifnya kazi za hapa na pale ili kujikumu kimaisha n ahata kulipa sehemu ya karo yake . Anasema kazi hizo nyingi hazikumruhusu kusoma vizuri ili ajitayarishe kwa mtihani na njia hiyo ya mkato ndio iliyokuwa bora kwake kuhakikisha kwamba hafeli katika mtihani .

Anasema kwamba alilazimika kulala na takriban wahadhiri watatu tofauti walioahidi kumpa alama za juu katika mtihani kwa sababu walifahamu kwamba hakuwa na muda wa kusoma .  Brenda anasema mtindo huo umekita sana mizizi katika vyuo  na taasisi za masomo ya juu na huenda itakuwa vigumu kuumaliza kabisa .