- Wanakijiji wanasema mshukiwa awali alikuwa amelalamika kwamba wazazi wake wanampenda sana kakake kumliko na kutishia kufanya jambo ambalo hakulieleza .
- Kibuyu cha petroli ,kisu na tochi vilipatikana katika boma hilo .mkuu wa DCI wa Mumias magharibi Robert Muriithi amekamatwa kwa uharibifu na sio kwa mauaji .
Mwanafunzi wa chuo kikuu amekamatwa kwa madai ya kuwachoma kwa moto kakake ,mke na mtoto wao katika kijiji kimoja huko Mumias ,kaunti ya kakamega .
Innocent Makokha anadaiwa kuichoma familia ya kakake katika nyumba yao huko Eshikalame wadi ya Musanda katika eneo bunge la mumias magharibi mapema siku ya jumamosi .
Eugene Omunyore, 23, mkewe Miriam Echesa na binti yao mwenye umri wa mwaka mmoja unusu walifaulu kukwepa kutoka nyumba yao iliyokuwa imeshika moto lakini walipata majeraha mabaya .
Walikimbizwa katika hospitali ya St Mary's Mission Hospital mjini Mumias ambako baadaye walihamishwa hadi Bungoma . Omunyore alifariki siku ya jumamosi ilhali binti yake aliaga dunia siku ya jumatatu .mke wake yungali amelazwa akiwa katika hali mbaya katika hospitali ya Life Care mjini Bungoma .
Wanakijiji wanasema mshukiwa awali alikuwa amelalamika kwamba wazazi wake wanampenda sana kakake kumliko na kutishia kufanya jambo ambalo hakulieleza .
Inadaiwa alirejea nyumbani siku ya jumamosi na kuanza kuchimba kaburi la kumzika kakake akizungumza lugh ambayo hakuna aliyeelewa . Kisha baadaye alipandwa na mori na kuanza kupasua madiridha ya vioo katika boma lao hatua iliyowafanya wazazi wake kuwaita polisi ambao walimkamata .
Polsi walimkamata siku ya jumatatu
" Nilisikia ukemi kutoka kwa wanangu wadogo wakitaka mlango ufunguliwe wakisema nyumba ya kaka yao ilikuwa ikiteketea .Nilipoamka niliona moto mkubwa umeifunika nyumba ake na nikatoka nje’ amesema Sella Atsieno, mamake marehemu Eugene
Atsieno amesema mshukiwa alikuwa akigombana naye pamoja na kakake kila mara na mara ya mwisho walipogombana ilikuwa siku nne zilizotangulia huku akiondoka baada ya kutoa onyo kwamba atafanya kitu kibaya .
Omunyore alirejea siku ya jumamosi baada ya kuwa nje kwa siku tatu na kuanza kumtukana pamoja na waliokuwa kwenye boma wakati huo huku akiwatishia kwa panga .Kisha alichukua jembe na kuanza kuchimba alichopsema ni kaburi la kakake.
Babake Omunyore Apollo Kalio amesema ukemi na kelele ziliwavutia majirani walioanza kusaidia kuuzima moto huo uliosambaa katika nyumba hiyo ya vyumba viwili .
Kibuyu cha petroli ,kisu na tochi vilipatikana katika boma hilo .mkuu wa DCI wa Mumias magharibi Robert Muriithi amekamatwa kwa uharibifu na sio kwa mauaji .