- Polisi wanatarajiwa kuwasilisha ombi la kutaka kumzuilia kwa muda wanapoendelea na uchunguzi wao .
- Mojawapo ya kisa hicho kinadaiwa kutokea katika shule moja ya watoto mtaani Buruburu mwaka wa 2019
Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko alilala seli jumatatu usiku na anatarajiwa kufikishwa kortini siku ya jumanne ili kujibu mashtaka mbali mbali .
Alichukuliwa siku ya jumanne asubuhi kutoka kituo cha polisi cha Muthaiga ambako alikuwa amelala usiku wa jumatatu na kupelekwa katika makao makuu ya DCI ili kuhojiwa .
Sonko, alitumia muda mwingi wa siku ya jumatatu katika afisi za DCI kwenye barabara ya Kiambu na anatarajiwa kufikishwa kortini baadaye leo .
Maafisa wanaofahamu kesi yake wanasema atakabiliwa na mashtaka saba ya wizi wa kimabavu na mashtaka matano ya kujeruhi .
Polisi wanatarajiwa kuwasilisha ombi la kutaka kumzuilia kwa muda wanapoendelea na uchunguzi wao .
Mojawapo ya kisa hicho kinadaiwa kutokea katika shule moja ya watoto mtaani Buruburu mwaka wa 2019
Siku ya jumatatu makachero walimhoji Sonko kuhusu matamshi yake kuhusiana na ghasia za uchaguzi wa 2017 . Sonko hata hivyo alikataa kuanikisha taarifa akisema amezuiwa na mahakama .
Ni wakati huo ambapo Sonko aliarifiwa na polisi kwamba hatoachiliwa huru kwa sababu kulikuwa na mashtaka mengine dhiidi yake .
Mawakili wake John Khaminwa, Assa Nyakundi, Evans Ondieki na George Kithi walikuwepo .
Juhudi zao za kutaka Sonko aachiliwe kwa dhamana ziliambulia patupu . Sonko aliagizwa kufika mbele ya DCI baada ya kudai kwamba yeye na katibu wa kudumu wa usalama wa ndani Karanja Kibicho walihusika na kupanga ghasia wakati wa uchaguzi wa 2017 kisha kukilaumu cha cha ODM kwa ghasia hizo .