Daktari ataka mahakama kuzuia ruzuku ya magari kwa MCA's

GHARAMA: Mwenyekiti wa SRC Lyn Cherop Mengich wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu marupurupu ya nyumba ya wabunge mnamo Mei 15, 2019. Picha: ENOS TECHE
GHARAMA: Mwenyekiti wa SRC Lyn Cherop Mengich wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu marupurupu ya nyumba ya wabunge mnamo Mei 15, 2019. Picha: ENOS TECHE

Daktari mmoja amemshtaki Rais Uhuru Kenyatta kwa kutumia pesa za umma kama chambo ili kupitisha muswada wa marekebisho ya katika chini ya mchakato wa BBI na akaomba korti isimamishe utoaji wa ruzuku ya gari kwa wakilishi wadi.

“Sio vibaya kwa mtu yeyote, pamoja na rais, kufanya kampeni kwa sababu fulani; shida ni kwamba rais anatumia fedha za umma kama ushawishi, ”Magare Gikenyi alisema.

"Kushindwa kwa Tume ya Mishahara kutekeleza jukumu lake na hivyo kutupilia mbali uhuru wake ili kufikia malengo ya serikali ili kuridhisha mabunge ya kaunti," ameongeza.

Kitendo cha serikali sio kwa masilahi ya umma na sio matumizi ya busara ya rasilimali chache za umma kuhakikisha uendelevu na usawa.

"Vitendo vya tume ya SRC ni kinyume cha sheria, sio kawaida na sio busara kusema machache na ni ya kibaguzi na ni matumizi mabaya ya ofisi ya umma kwa manufaa ya kibinafsi tofauti na huduma kwa watu," Gikenyi alisema.

Alisema kwa uhuru wa tume ya SRC sio sio hundi wazi kwa tume hiyo kuamua kufanya chochote kinachowapendeza  'marafiki wao.

"Uhuru huja na majukumu, uwajibikaji, uwazi, sheria na kanuni," alisema.

Daktari huyo alisema maafisa wengi wa umma wanaowahudumia Wakenya wana mikopo ya magari ambayo haijabadilishwa kuwa ruzuku na hakuna kitu maalum wakilishi waydi wanafanyia wakenya kustaohili ruzuku ya magari.

"Kwa mara moja, wacha tuketi tujiulize, kwa nini tunazungumza juu ya magari wakati kuna mambo makubwa zaidi katika jamii yetu? Jamii yetu imekumbwa na janga la Covid-19. Watu wetu wamepoteza kazi, tegemeo katika familia wanajitahidi kupata riziki.

Deni letu la nje limegonga Shilingi trilioni 8.4; uchumi wetu umedorora hadi kati ya asilimia 1-1.5, ”alisema.