Haya hapa mambo wanawake wanahitaji kufanyiwa na waume wao lakini hawatasema

Muhtasari

Haya hapa mambo wanawake wanahitaji kufanyiwa na waume wao lakini hawatasema

Kuna wale hufanya mambo hayo na wanayafahamu vyema ilhali kuna wale hawajui wala kusoma vitendo vya wake zao

Ni matamanio ya kila mwanamke kudekezwa kama mtoto katika uhusiano wa kimapenzi.

Kuna baadhi ya mambo ambayo wanawake wengi hutaka kufanyiwa na waume wao kila usiku lakini ni ngumu sana kwao kusema lakini watakuonyesha kwa vitendo.

Kuna wale hufanya mambo hayo na wanayafahamu vyema ilhali kuna wale hawajui wala kusoma vitendo vya wake zao.

Haya hapa baadhi ya mambo hayo;

1.Tazama filamu naye usiku

Baada ya kuchoka mchana mzima kuna wanawake ambao watataka wapumzike na waume wao au wapenzi wao na kutazama filamu pamoja.

Kuna baadhi ya wanaume wataenda na marafiki zao kutazama filamu pamoja na kusahau kama wana wake

Haya basi siri ndio hii tazama naye kwa maana ni wa maana katika maisha yako.

2.Kwa mara moja mpikie

Ndio wanawake wengi wanafahhamika kwa upishi wo, lakini siku moja mshangaze na kumwambia mpenzi pumzika leo nikupikie.

Mwanamke wao atahisi kwamba ameangukia kuwa na mwanamume kama wewe.

3.Kila unaporudi kutoka nyumbani mpe busu la shavu

Baadhi ya wanaume watafika ata salamu hawatampa mke wake kazi nikuuliza kama mna chakula au chai ya jioni.

Ukimpa mapenzi tele kwa kweli atashukuru, siri ya wanawake baadhi yao ushukuru yale kidogo umemfanyia.

4.Muoshe miguu kila usiku

Pasha maji moto mwambie aketi chini uweze kumuosha miguu,na kumsakata vyema ili uchovu uishe.