Kwanini corona iliwafichua wasichana wa shule ambao ni wajawazito

Muhtasari
  • Kwanini corona iliwafichua wasichana wa shule ambao ni wajawazito
  • Visa vya unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji wa nyumbani viliongezeka sana wakati huo ambao haujawahi kutokea
  • Kutoka kwa utafiti uliofanywa na N.G.O unaonyesha kuwa ujauzito wa utotoni umekuwa athari mbaya ya janga hilo
student
student

Tangu shule zilifungwa kwa muda wa miezi kumi  baada ya visa vya kwanza vya janga kuathiri nchi yetu, wasichana wadogo wa shule walikuwa windo rahisi kwa wanaume wasio na maadili.

Visa vya unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji wa nyumbani viliongezeka sana wakati huo ambao haujawahi kutokea.

Kutoka kwa utafiti uliofanywa na N.G.O unaonyesha kuwa ujauzito wa utotoni umekuwa athari mbaya ya janga hilo.

Licha ya hatua kali za Rais juu ya kuongezeka kwa visa vya ujauzito kati ya wasichana wa shule, kesi hizi hazikuonekana kusimama.

Wasichana wengi wadogo wananyanyaswa nchi nzima kingono na jamaa zao wa karibu au majirani.

Wakuu na tawala za mitaa walipewa mamlaka ya kuongezeka kwa kesi hizi na pia kuhakikisha wale waliohusika wanashtakiwa kulingana na sheria za nchi.

Asilimia kubwa ya wasichana wadogo hawakurudi shule kuendeleza masomo yao baada ya shule kufunguliwa.

Wengi wao hawafahamu wala kujua jinsi walivyojipata katika mtego huo.

Huku niikizungumza na baadhi ya wasichana hao walikuwa na haya ya kusema.

Monicah ambaye si jina lake halisi alisema kwamba,

"Kwa kweli sijui jinsi nilipata katika mtego huu, niko katika kadato cha pili.baada ya corona kuingia nchini na tukafunga shule tumekuwa na muda mwingi wa kuharibu

Ndio utapata tunasoma lakini akili haiko kwa masomo, nilienda kuambia mwenye jukumu la ujauzito wangu, lakini aliniambia niavye mimba yenyewe

Nilikataa na nikasema wacha yatokee yale yatayotokea,siwezi avya mimba ili nionekane mzuri, ndio nitasimamisha masomo yangu ili nimlee mtoto wangu

Lakini mtoto wangu akikua nitarudi na kuendelea na masomo yangu, wazazi wangu waligadhabishwa sana na kitendo changu

Baba yangu alinifukuza kwa muda nikaenda kuishi kwa shhangaziyangu hadi pale hasira zilikwisha

biliwaomba msamaha wakanisamehe, wazazi wangu tangu nifunge shule nilikuwa nawaona tu usiku wakitoka kazi," Alizungumza Monicah.

Mwanafunzi huyo pia alikuwa na rafiki yake ambaye pia alijipata katika mtego huo.

"Kwa majina naitwa shantel, niko katika darasa la nane, wazazi wangu walikasirika sana walipogundua kwamba nina ujauzito

Licha yangu kuwa na umri wa miaka 13, nilijipata katika mtego huu bila ya kujua lakini nina imani kwamba nitajifungua vyema na niendelee na masomo yangu," Aliongea mwanafunzi huyo.

Baada ya kuzungumza na wanafunzi hao nilizungumza na mmoja wa wazazi wao ambaye alionekana na masikitiko makubwa sana baada ya msichan wake kubeba ujauzito.

"Kwa kweli nimesikitika sana kwa yale ambayo tunaona wasichana wa shule wanapitia na hata kujiingiza

Mimi nilikuwa nalea Monicah nikiw pekeyangu, nilifanya kazi juu chini kuhakikisha kwamba hajafukuzwa shule kwa ajili ya karo

Kwa nyumba kulikuwa na kila kitu, licha yangu kufanya bidii kazini, ndio sikuwa na muda wa kutosha na watoto wangu, kwa sababu sikutaka walael njaa au wakirudi shule wakose karo

Kile ambacho nawea kuwahimiza wazazi wawafunze watoto wao hasa wasichana kuhusu ngono na kutenga muda wao wakae na watoto wao

Monicah kama ataamua kurudi shule baada ya kuzaa ndio nitamkubali, kwa maana hii nchi bila hati ttofauti za masomo wewe si mtu, sikuwa nataka apitie maisha amabayo nimepitia," Alizungumza.

Haya basi hizi hapa baadi ya sababu kwanini corona imewafichua wasichana wa shule ambao ni wajawazito.

1.Wazazi wasiowajibika

Baada ya kuchunguza kwa muda wazazi wengi hawajibiki katika kuwafunza wasichana wao kuhusu jamii ya hapa nje, na bora si masomo tu ya shule, wazazi wengi wana kauli ya kwamba 'bora mtoto wangu ameshiba na hajafukuzwa shule hayo mengine ni kelele'

Wengi ambao wanatumia kauli hiyo wamejipata wakijuta kila kuchao.

2.Ukosefu wa Mafunzo ya ngono

Wasichana wengi hasa mashinani hawapokei mafunzo ya ngono, hawajui wala kufahamu nini haswa kitatokea baada ya kufanya ngono ukiwa na umri mchanga.

3.Akili isiyo na kazi

Baada ya shule kufungwa wanafunzi wengi hawakushika vitabu wala kujihusisha na mafunzo tofauti kanisani, akili ya wanafunzii wengi zilikuwa hazina kazi zimetulia.

Na biblia inasema 'Idle mind always thinks evil'.

4. Jamii zetu

Katika jamii zetu hasa katika karne hii ya sasa tumechukulia ngono kama jambo la kawaida na kusahau kuwa tuna wanafunzo ambao wanahitaji mafunzo yetu kuhusu ngono.

Kwa kuwahimiza wasichana waliojipata katika mtego wa ujauzito wakati huu mgumu ambapo tunapambana na janga la corona ni kuwa sio mwisho wa dunia, unaweza kujifungua na kurudi shuleni na wala wasirudie makosa hayo tena.