'Usha anza kujipendekeza,'Watanzania wamuuliza Harmonize baada ya kutoa kibao akimsifu Rais Samia

Muhtasari
  • Wanamitandao wamkejeli Harmonize baada ya kutoa kibo chake kipya 
  • Katika wimbo mpyaamewaacha wafuasi wake wengi wakiwa na mshtuko
  • Ametoa wimbo wa kumsifu rais wa sasa wa Mtanzania, Samia Suluhu Hassan
68982464_381056136120833_6438164767961324750_n
68982464_381056136120833_6438164767961324750_n

Msanii wa nyimbo za aina ya bongo Flava kutoka Tanzania Harmonize, siku ya Jumamosi alitoa kibao kinachofahamika kama 'Tuvushe'.

Katika wimbo mpyaamewaacha wafuasi wake wengi wakiwa na mshtuko.

Ametoa wimbo wa kumsifu rais wa sasa wa Mtanzania, Samia Suluhu Hassan.

Wimbo mpya unaitwa 'Tuvushe', na ujumbe kuu ambao Harmonize alikuwa akipitisha ni kwamba ukuu wake Rais Samia ataipeleka Tanzania katika ngazi nyingine, kutoka alikotoka rais wa zamani  hayati John Pombe Magufuli.

Watanzania walimdhihaki wakimwambia kwamba alifanya hivyo kwa sababu alitaka kupata kibali machoni pa Rais Suluhu, wazo ambalo wengi wao walitaja kitendo chake kama nguvu.

Hizi hapa baadhi ya hisiaza za wanamitandao;

rose.: mapenziUsha anza kujipendekeza

deborah_cutie: 😂😂😂😂😂😂 bendera fwata upepo

ficloveofficial: Mama SAMIA SULUHU

amiryjanja: Safiiiiiiii we ndio huwa unaanza na wengine hufuta

kondegangmuseum: Kujituma ndio siri ya mafanikio katika maisha❤️❤️❤️❤️

bongomaudaku: Hii Nyimbo Mbaya Alafu UCHAWA WA SIASA NA WEWE NI MSANII NI TATIZO KUBWA 😢😢😢